Jinsi ya Kustahili Kupokea Msaada wa FEMA Wakati wa Majanga: Matakwa ya Uraia na Uhamiaji

FEMA na serikali ya jimbo, eneo au kabila inaweza kutoa msaada wa moja kwa moja na wa kifedha kwa raia wa Marekani, wananchi ambao si raia, na waliotimiza vigezo ingawa si raia.

Msaada wakati wa janga unaweza kutia ndani kupata pesa kwa ajili ya kulipia kodi kwa muda mfupi, kurekebishiwa nyumba, mali ya kibinafsi iliyopotea, matibabu, gharama za mazishi, na mahitaji au gharama nyingine kubwa zinazohusiana na janga lililotokea ambazo hazishughulikiwi na bima au njia nyingine.

Waathiriwa wa janga, haijalishi hali yao ya uraia na uhamiaji, wanaweza kupokea huduma zifuatazo ikiwa zinapatikana: rasilimali za kutegemeza uhai kama vile makazi, chakula na maji, ushauri wa jinsi ya kukabiliana na janga, kushughulikia hali za majanga, kupokea lishe ya ziada na huduma za kisheria.

Ufafanuzi

Raia wa Marekani

Mtu yeyote aliyezaliwa Marekani; mtu yeyote aliyezaliwa nje ya Marekani ambaye angalau mzazi wake mmoja ni Mmarekani; au raia wa asili.

Mwananchi Ambaye si Raia

Mtu aliyezaliwa Samoa ya Marekani au Kisiwa cha Swain kwenye tarehe ambayo Marekani ilimiliki maeneo hayo na pia baada ya tarehe hiyo, au mtu ambaye wazazi wake ni wananchi wa Marekani ambao si raia. Raia wote wa Marekani ni wananchi wa Marekani, lakini si wananchi wote wa Marekani ni raia wa Marekani.

Watu Waliotimiza Vigezo Ingawa si Raia Hujumuisha

  • Mkaazi wa Kudumu Kisheria (aliye na “Green Card”)
  • Watu ambao si raia waliopewa hifadhi
  • Wakimbizi
  • Watu wasio raia ambao hali yao ya kufukuzwa imezuiliwa kwa angalau mwaka mmoja
  • Watu wasio raia walioachiliwa kwa masharti nchini Marekani kwa angalau mwaka mmoja kwa sababu ya dharura ya kupokea msaada wa kibinadamu au manufaa kubwa ya umma
  • Wahamiji kutoka Cuba/Haiti
  • Watu fulani wanaopigwa ambao si raia, au wenzi wao au watoto
  • Baadhi ya watu walioathiriwa na biashara mbaya ya usafirishaji binadamu, kutia ndani wale ambao visa yao ina alama “T” au “U”
Graphic
Mixed group of people standing.

Ikiwa mwombaji hajatimiza matakwa ya uraia au uhamiaji wakati anapojaza ombi, familia inaweza kujaza ombi la kupokea msaada fulani kutoka kwa serikali ikiwa:

Mzazi au mlezi wa kisheria wa mtoto mdogo ambaye ni raia wa Marekani, mwananchi ambaye si raia au waliotimiza vigezo vya uraia ingawa si raia wanaweza kujaza ombi la kupokea msaada kwa niaba ya mtoto, maadamu wanaishi katika nyumba moja. Mzazi au mlezi wa kisheria anapaswa kujaza kama mwombaji-mwenza, na mtoto anapaswa kuwa chini ya miaka 18 wakati janga linapotokea.

Watu wote walioathiriwa na janga kubwa, haijalishi uraia wao au hali yao ya uhamiaji, wanaweza kupokea msaada wa ushauri wa jinsi ya kukabiliana na janga, huduma za kisheria zinazohusiana na janga, kushughulikia hali za janga, lishe ya ziada wakati wa janga, na misaada mingine isiyo ya kipesa inayotolewa wakati wa dharura ya janga. Inatia ndani matibabu, makazi, chakula na maji.

Vyanzo vya Misaada

alert - warning

Mtu anapaswa kwenda kwa maofisa wa uhamiaji ili wamsaidie kujua ikiwa ametimiza matakwa ya uhamiaji yatakayomwezesha kupokea msaada wa FEMA wakati wa majanga.

Pia, mashirika mengine ya kujitolea hutoa misaada bila kujali hali ya uraia au uhamiaji.

Watu wote walioathiriwa na janga kubwa, haijalishi uraia wao au hali yao ya uhamiaji, wanaweza kupokea msaada wa ushauri wa jinsi ya kukabiliana na janga, huduma za kisheria zinazohusiana na janga, kushughulikia hali za janga, lishe ya ziada wakati wa janga na misaada mingine isiyo ya kipesa inayotolewa wakati wa dharura ya janga. Inatia ndani matibabu, makazi, chakula na maji.

Tembelea Ukurasa wa Mashirika ya Kujitolea ili upate habari zaidi.

Ilisasishwa mara ya mwisho