Hifadhi Vitu Vyenye Thamani Vya Familia

Hifadhi Vitu Vyenye Thamani Vya Familia

Madokezo ya Haraka

Ithibati

Rasilimali za Ziada

FEMA na Smithsonian Institution zinafadhili kwa pamoja Jopo la Dharura la Kitaifa la Heritage, muungano wa zaidi ya mashirika 60 ya kutoa huduma za kitaifa na mawakala wa kiserikali uliobuniwa ili kulinda itifaki za kitamaduni kutokana na madhara ya majanga ya kiasili na hali zingine za dharura.

Jopo hilo hutoa mwongozo ufuatao ili kukuwezesha kupata tena vitu vyenye thamani vya familia yako baada ya janga.

Hatua za Kuhifadhi Vitu Vyenye Thamani Vya familia Yako

Ukiwa na subira kidogo na kuchukua hatua mara moja, inawezekana kuhifadhi picha zinazopendwa, barua, michoro na vitu vingine vya pekee usivyoweza kuvipata vikipotea. Maagizo haya ya hatua kwa hatua yatakusaidia kuhifadhi vitu vyako vyenye thamani na kukupatia fursa ya kufanya uamuzi mzuri wa kushughulikia kumbukumbu za familia yako.

 1. Anza na Kilicho Muhimu Zaidi: Huenda usiweze kuhifadhi kila kitu, kwa hivyo kazia uangalifu kilicho muhimu zaidi kwako, iwe ni kwa sababu za kihistoria, kifedha, au hisia za kuhuzunisha.
 2. Buni Nafasi: Kutandaza vitu ili vikauke huchukua nafasi kubwa! Uwe mbunifu: kwa utaratibu ning’iniza picha kwenye kamba za kuanika nguo, tengeneza kifaa cha kukaushia kutokana na vifaa vya plastiki vilivyofungwa kati ya viti viwili, ziba nafasi kwa kitambaa au funga vining’inizo hivyo kwa paipu (pipe) ili kuziimarisha zaidi
 3. Shika kwa Uangalifu: Uwe mwangalifu zaidi unaposhika vifaa vya itifaki ya kifamilia, ambavyo vinaweza kuwa hafifu vikiwa na unyevu.

Madokezo ya Haraka

Kukausha polepole kwa hewa ni bora kwa vitu vyako vyote vyenye thamani—ndani ya nyumba, ikiwezekana. Mashine za kukausha nywele, pasi, majiko ya kuokea, na kuweka kwenye jua kwa muda mrefu kutasababisha madhara yasiyoweza kurekebishwa. Ongeza kiasi cha hewa inayoingia ndani ya nyumba kwa kutumia vifaa vya kupiga hewa (fans), fungua madirisha, viyoyozi, na vifaa vya kumaliza unyevuvyevu.

Picha, stakabadhi, vitabu, na vitambaa vinapaswa kuwekwa ndani ya friji iwapo huwezi kuzikausha ndani ya saa 48. Zifunge kwa karatasi ya kuhifadhia ndani ya friji kisha uziweke ndani ya friji isiyo na barafu na uweke kiwango cha joto cha chini zaidi iwezekanavyo.

Picha

 • Kamwe usitenganishe kwa kuvuta picha zilizoshikamana.
 • Wakati ukiruhusu, ipige picha picha hiyo ili uhifadhi nakala yake ya kidijitali
 • Safisha picha kwa kuzipitisha kwa uangalifu kwenye maji yaliyochujwa, ikiwa yanapatikana, au kwenye maji safi ikiwa huwezi kupata maji yaliyochujwa.
 • Kausha picha kwenye hewa kwa kutumia skrini ya plastiki au kitambaa, au kwa kuzining’iniza kwa kuzishika kwenye ncha kwa kutumia pini za plastiki za nguo.
 • Usiache upande wenye picha ushikamane na vitu vingine inapoendelea kukauka.

Habari za Ziada Katika PDF

Vitabu

 • Iwapo una vitabu vilivyokuwa kwenye maji-taka, ni hatari kwa afya yako. Viharibu au umwombe ushauri mhifadhi mwenye ujuzi.
 • Ondoa jaketi za vumbi ili zikauke zikiwa kando.
 • Weka kitambaa katikati ya kurasa za vitabu vilivyo na unyevu.
 • Kuhusu vitabu vilivyo na unyevu au unyevu kidogo, ikiwa vitabu vilikuwa kwenye matope, kutu, au maji yenye chumvi, yamwagilie maji, moja baada ya kingine, ndani ya ndoo au beseni lenye maji safi, huku ukikifinya kitabu kwa nguvu ukiwa umekifunga unapokitumbukiza ndani.

Habari za Ziada Katika PDF

Stakabadhi, Michoro na Karatasi

 • Ondoa rangi na maandishi kutoka kwenye fremu.
 • Kausha vitu kwenye hewa ikiwa una stakabadhi chache tu zenye unyevu au karatasi, au iwapo una nafasi ya kutosha kukaushia bidhaa zako zote.
 • Kausha kwa kutumia hewa zikiwa moja moja mahali tambarare au katika vifurushi vidogo vya hadi robo inchi kwenda juu.
 • Stakabadhi zinaweza kuhifadhiwa kwa barafu ikiwa una vipande vingi sana visiweze kukaushwa kwa jua. Mbinu hii inaweza kuchukua majuma hadi miezi kadhaa.

Habari za Ziada Katika PDF

Hati za Ithibati

Watu wanapoathiriwa na mafuriko, kimbunga, tufani au moto, vitu vyenye thamani kama vile itifaki za kifamilia, picha na vifaa vingine vinakuwa vyenye thamani sana Jopo la Kitaifa la Dharua la Heritage huandaa miongozo hii ya msingi kutoka kwa wahifadhi wenye ujuzi kwa ajili ya wale ambao wanatafuta — na kupata — vitu vya thamani vya familia licha ya uharibifu.

Baada ya Moto: Ushauri wa Kuokoa Vitu Vya Thamani Vya Familia Vilivyoharibika

Baada ya Furiko: Ushauri wa Kuokoa Vitu Vya Thamani Vya Familia Vilivyoharibika

Kuokoa Vitu Vya Thamani Vya Familia Vilivyoharibiwa na Maji

Habari za Ziada

Tangu mwaka wa 1995, Jopo hilo limekuwa likiwaandalia watu na jamii za kitamaduni – makavazi, maktaba, hifadhi za vitu vya kale, mashirika ya sanaa, ofisi za kuweka rekodi na zaidi – mwongozo na msaada wa kiufundi kabla, wakati na baada ya majanga.

Hazina kubwa ya habari inapatikana katika tovuti ya Jopo hilo, kutia ndani yafuatayo:

Kwa habari zaidi kuhusu kulinda itifaki za kitamaduni zilizohatarishwa au zilizoathiriwa na majanga — Marekani na ughaibuni — tembelea tovuti ya mshirika wetu, Smithsonian Cultural Rescue Initiative.

Ilisasishwa mara ya mwisho