Jitolee & Utoe Mchango

Baada ya janga watu huungana ili kusaidia. Ili mchango wako uwe wenye manufaa zaidi, ni muhimu kufuata miongozo ya kuchanga na kujitolea kwa njia inayoonyesha uwajibikaji. Hapa chini kuna hatua zilizojaribiwa na zilizo sahihi zitakazokupa mwanzo mzuri. 

Unaweza kutuma barua pepe kwa Kitengo cha Michango cha FEMA ili kupata majibu kwa maswali yako hususa au kutoa mchango wako ambao si hela.

Hela ni Bora

Michango ya kifedha kwa mashirika yanayojulikana ya kuandaa misaada kunapokuwa na majanga ndiyo njia ya haraka zaidi, inayonyumbulika zaidi, na yenye matokeo zaidi ya kutoa michango. Mashirika yaliyo kwenye eneo la janga yanajua bidhaa na viwango vinavyohitajika, mara nyingi yananunua kwa wingi na kupata punguzo na, inapowezekana hununua kwa biashara zilizo kwenye eneo la janga, na hivyo kutegemeza urudishaji wa awali wa hali ya kiuchumi.

Michango isiyohusisha hela: Hakikisha ni Nini, Wapi na Wakati Gani

Bidhaa zilizochangwa zinahitajika. Hata hivyo, kusipokuwa na mpangilio uliofikiriwa vizuri, bidhaa zilizochangwa zinaweza kulemaza jamii iliyo katika hali ngumu tayari. Kujua kile kinachohitajika, mahali kinapohitajika, na kukifikisha hapo kwa wakati unaofaa ndilo jambo muhimu. Mahitaji muhimu hubadilika haraka. Kabla ya kuzikusanya hakikisha kwamba uhitaji upo.

  • Si kila kitu kinachohitajika. Nguo zilizotumika huwa hazihitajiki kamwe. 
  • Michango mikubwa ni bora zaidi. Weka kwenye masanduku ya mbao mizigo ya aina moja, iliyochaguliwa, na kuwekwa ndani ya vijisanduku.
  • Kuzingatia muda ni muhimu. Hakuna anayefaidika ikiletwa mapema sana au kuchelewa mno.
  • Usafiri unapaswa kufanyiwa kazi. Itafikaje mahali inapohitajiwa?

Jiunge na Mjitoleaji

alert - warning

Usijipeleke kwa maeneo ya majanga.

Mashirika yanayoaminika yanayoendesha shughuli katika eneo lililoathiriwa yanajua ni wapi wajitoleaji wanahitajiwa. Ikitegemea janga na ni wapi hasa janga limefikia, wajitoleaji wanaweza kuandaa msaada mkubwa ili kuhakikisha manusura wanaweza kurudia maisha yao mapya ya kawaida. Kwa kufanya kazi na shirika lisilo la kibiashara, stadi zinazofaa za usalama, mafunzo na ufundi zinaweza kuzingatiwa.

Kurudisha hali ya awali huchukua muda mrefu zaidi kuliko umakinifu wa vyombo vya habari. Kutakuwa na uhitaji wa wajitoleaji kwa miezi mingi, mara nyingi miaka mingi, baada ya janga.  Mara nyingi msaada wako huhitajika muda mrefu baada ya janga.

Jinsi Unavyoweza Kusaidia

Graphic
An email icon.

Ikiwa una bidhaa za kuchangia, muda wa kujitolea ili kutegemeza shirika lisilo la faida, au hela za kutoa na una maswali, tuma barua pepe kwa Kitengo cha Michango cha FEMA. Tungependa kukusaidia, uwasaidie wengine.

Ili kupata orodha ya mashirika yanayotegemeka, habari za ziada kuhusu michango na rasilimali zingine, tembelea . Mashirika ya Kitaifa ya Kujitolea Yanayofanya kazi katika Majanga.

Ilisasishwa mara ya mwisho