This page has not been translated into Swahili. Visit the Swahili page for resources in that language.
Fact Sheets
FEMA ilitekeleza sasisho muhimu zaidi kwa msaada wa maafa katika miaka 20 iliyopita.
Dhoruba za hivi majuzi za Vermont zinaonyesha kiasi cha uharibifu ambayo mafuriko yanaweza kusababisha. Kulinda nyumba au biashara yako kutumia sera kutoka kwa Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Mafuriko kunaweza kukusaidia kujiandaa kwa ajili ya - na shughuli za urejesho baada ya - mafuriko wakati ujao.
Manusura wa majanga katika kaunti za Caledonia, Chittenden, Lamoille, Orange, Orleans, Rutland, Washington, Windham na Windsor waliotuma maombi ya msaada kutoka kwa FEMA kwa ajili ya dhoruba kali za Julai, mafuriko, maporomoko ya ardhi na matope watapokea barua ya uamuzi wa ustahilifu kutoka kwa FEMA kupitia barua au barua pepe.
Kama sehemu ya mchakato wa msaada wa majanga FEMA lazima ibainishe umiliki na ukaaji wa makazi ya msingi yaliyoharibiwa. FEMA imerahisisha uthibitishaji wa umiliki na ukaaji kwa ajili ya manusura wa majanga katika kaunti za Caledonia, Chittenden, Lamoille, Orange, Orleans, Rutland, Washington, Windham na Windsor ambao walipata hasara kutokana na dhoruba kali za Julai, mafuriko, maporomoko ya ardhi na matope. Wamiliki na wapangaji lazima wathibitishe kuwa walikaa katika makao ya msingi yaliyoharibiwa na majanga kabla ya kupokea Msaada wa Makao na baadhi ya aina za Msaada wa Mahitaji Mengine. FEMA sasa inakubali hati nyingi tofauti tofauti.
Mara tu unapotuma ombi la msaada wa FEMA, unapaswa kuwasilisha dai la bima ikiwa bado hujafanya hivyo. FEMA inaweza kuwasiliana nawe ili kuthibitisha habari au kukamilisha ukaguzi wa nyumba, na inaweza kukutuma kwa Usimamizi wa Biashara Ndogo ya Marekani. FEMA inaposhughulikia ombi lako, utapokea barua ya uamuzi, ambayo unaweza kukata rufaa.
Unapotuma ombi la msaada wa majanga, lazima FEMA ithibitishe utambulisho wako ili kuhakikisha kuwa unapokea msaada unaostahili. Ikiwa FEMA haiwezi kuthibitisha utambulisho wako kupitia rekodi za umma, unaweza kuhitajika kuwasilisha hati za ziada.
FEMA mara nyingi huwatuma manusura wa majanga kwa Usimamizi wa Biashara Ndogo ya Marekani (SBA) ili kutuma maombi ya mikopo ya majanga yenye riba nafuu. Mikopo ya majanga ni sehemu muhimu ya msaada wa serikali, na inaweza kusaidia wamiliki wa nyumba, wapangaji, biashara za ukubwa wowote na baadhi ya mashirika yasiyo ya kibiashara kurejelea hali ya awali.
Wamiliki wa nyumba na wapangaji wa Vermont katika kaunti za Caledonia, Chittenden, Lamoille, Orange, Orleans, Rutland, Washington, Windham na Windsor ambao waliathiriwa na dhoruba kali, mafuriko, maporomoko ya ardhi na maporomoko ya udongo yaliyotokea kuanzia Julai 7, 2023, na kuendelea wanaweza kustahili ufadhili wa FEMA kwa ajili ya hasara ya mali ya kibinafsi na gharama zingine zinazostahili.
Kujiandikisha ili kupata msaada wa majanga kutoka kwa FEMA hakutaathiri ustahilifu wako wa udhamini mwingine wa serikali.
FEMA inaweza kutoa aina mbili za msaada kufuatia tamko la majanga la rais: Msaada wa Mtu Binafsi na Msaada wa Umma. Programu hizi mbili zinafadhiliwa kando kando na zinakusudiwa kufaidi watu binafsi na jamii kwa njia tofauti.