Msaada Unaowezekana wa Makao na Nyumba kwa Waathiriwa wa Janga

Waathiriwa wa janga ambao makao yao ya msingi yaliharibiwa wanaweza kustahili Msaada wa Makao na Nyumba wa FEMA.

Msaada wa Kukodisha

Msaada wa Muda wa Makao

Kukarabati/Kubadilisha Nyumba

Makazi ya Muda ya Moja kwa Moja

Msaada wa Kukodisha

Pesa zinaweza kupatikana kwa waathiriwa wanaostahili ambao wanahitaji mahali pa kuishi kwa muda wakati nyumba yao inaporekebishwa, au hadi wapate makazi ya kudumu.

Ni Nani Anayeweza Kustahili?

Mwathiriwa wa janga:

  • Ambaye nyumba yake haiwezi kukaliwa kutokana na janga
  • Anayekubali kuhama
  • Ambaye mahitaji yake ya nyumba hayalipwi na bima

Jifunze jinsi ya kuwasilisha ombi.

Graphic
An apartment building.

Msaada wa Muda wa Makao

Ikiidhinishwa kwa ajili ya janga, FEMA inaweza kuandaa makazi ya muda kwa waathiriwa wa janga wanaostahili kwa kutumia hoteli zinazoshiriki.

Ni Nani Anayeweza Kustahili?

Mwathiriwa wa janga:

  • Ambaye amehamishwa na kukimbilia katika maeneo ya dharura
  • Ambaye nyumba yake haiwezi kukaliwa au haifikiki kwa sababu ya janga

Iwapo bado hujawasilisha ombi la Msaada, jifunze jinsi ya kuwasilisha ombi.

Graphic
A hotel.
alert - info

Iwapo umekamilisha ombi la Msaada wa janga la FEMA, utazingatiwa kwa Msaada wa Muda wa Makao (TSA) ikiwa mpango utaidhinishwa na serikali ya jimbo, eneo au kabila lako. FEMA itakuarifu ikiwa unastahili kuwa katika mpango huo.

Kukarabati/Kubadilisha Nyumba

Msaada wa kifedha unaweza kupatikana kwa wamiliki wa nyumba wanaostahili ili kujenga upya au kufanya ukarabati wa msingi ili nyumba zao ziwe salama, safi na zenye kutumika.

Ni Nani Anayeweza Kustahili?

Mmiliki wa nyumba:

  • Ambaye makazi yake ya msingi yamebainika kuwa haiwezi kukaliwa baada ya ukaguzi wa FEMA
  • Ambaye mahitaji yake ya makao haishughulikiwa na bima

Jifunze jinsi ya kuwasilisha ombi.

Graphic
A house with a cloud over it with water in front of it.

Makazi ya Muda ya Moja kwa Moja

Msaada wa aina hii huandaa matumizi ya muda ya vitengo vya makazi vinavyoweza kusafirishwa vilivyotolewa na FEMA kwa waathiriwa wanaostahili.

Ni Nani Anayeweza Kustahili?

Mwathiriwa wa janga:

  • Ambaye nyumba yake ya msingi imeharibiwa au haiwezi kukaliwa kutokana na uharibifu mkubwa uliosababishwa na janga
  • Ambaye hana chaguo lingine la makazi ya muda linalopatikana ndani ya umbali unaokubalika wa kusafiri kwa sababu ya ukosefu wa rasilimali za kukodisha.

Jifunze jinsi ya kuwasilisha ombi.

Graphic
A trailer.
Ilisasishwa mara ya mwisho