Taarifa kwenye ukurasa huu haionyeshi masasisho ya Usaidizi wa Mtu Binafsi kwa majanga yaliyotangazwa mnamo au baada ya tarehe 22 Machi, 2024.
Jifunze zaidi kuhusu kile kinachopatikana sasa.
Mpango wa Watu Binafsi na Familia (IHP) hutoa huduma za kifedha na za moja kwa moja kwa watu binafsi na familia zinazostahili zilizoathiriwa na janga, ambazo hazina bima au hazina bima ya kutosha ya gharama muhimu na mahitaji makubwa. Msaada wa IHP si mbadala wa bima na hauwezi kufidia hasara zote zinazosababishwa na janga. Msaada huo unakusudiwa kukidhi mahitaji yako ya msingi na kusaidia katika juhudi za uokoaji wa janga.
FEMA imejitolea kuandaa ufikiaji sawa wa rasilimali na Msaada wa kurejesha baada ya janga. Ijulishe FEMA ikiwa wewe au mtu yeyote katika familia yako ana ulemavu au uhitaji wa lugha.
Msaada wa IHP unaweza kujumuisha:
- Fedha za makazi ya muda wakati ambapo huwezi kuishi nyumbani mwako, kama vile Msaada wa kukodisha au ulipaji wa gharama za hoteli.
- Kitengo cha makazi ya muda, ikiwa kimeidhinishwa kwa janga, wakati ambapo huwezi kutumia msaada wa kukodisha kwa sababu ya ukosefu wa rasilimali za nyumba zinazoweza kupatikana.
- Pesa za kusaidia kukarabati au kubadilisha nyumba zinazokaliwa na wamiliki ambazo zinatumika kama makazi ya msingi ya familia, ikijumuisha njia za kufikia zinazomilikiwa na watu binafsi, kama vile njia za kuingia, barabara au madaraja.
- Fedha za msaada wa kupunguza hatari ili kusaidia wamiliki wa nyumba wanaostahili kukarabati au kujenga upya nyumba zenye nguvu na zinazodumu zaidi
- Fedha kwa ajili ya gharama nyingine zisizo na bima au zisizo na bima ya kutosha zinazosababishwa na janga na mahitaji makubwa
Sheria kuhusu Faragha inaitaka FEMA kupata idhini iliyoandikwa kutoka kwa mwombaji ili kushiriki rekodi zao za Msaada wa janga na wahusika wengine. Waombaji wanaotaka kuidhinisha FEMA kushiriki maelezo yao na wahusika wengine lazima wajaze FOMU ya FEMA FF-104-FY-21-118: Uidhinishaji wa Utoaji wa Taarifa Chini ya Sheria ya Faragha na kuzirejesha kwa FEMA.
Jifunze Kuhusu Msaada wa FEMA IHP
- Pata maelezo zaidi kuhusu Msaada wa Makazi na Nyumba ya FEMA ambayo huenda ukastahili kupokea.
- Kuelewa vigezo vya jumla vya kustahili ambavyo vinahitaji kufikiwa ili kupokea Msaada.
- Jifunze kuhusu matakwa ya uraia na hali ya uhamiaji kwa manufaa ya serikali ya umma.
- Kagua msaada unaotolewa na FEMA kwa familia na mahitaji mengine.
- Jifunze jinsi ya kuwasilisha ombi la Msaada mtandaoni, kwa simu au ana kwa ana.
Waombaji wanaohitaji Msaada Unaoendelea wa Makazi ya Muda wanaweza kuomba Msaada wa ziada kwa kukamilisha FEMA Form FF-104-FY-21-115: Ombi la Msaada Unaoendelea wa Makazi ya Muda na kuirejesha kwa FEMA Pamoja na hati tegemezi.
Mipango Mingine ya Msaada
Zaidi ya nyumba, FEMA ina programu nyingine za Msaada wa Mtu Binafsi zilizoundwa kusaidia waathiriwa wa janga, kama vile Msaada wa Kukosa Ajira wakati wa Janga, Ushauri wa Migogoro, Huduma za Kisheria Wakati wa Janga na zaidi.