Jinsi ya Kumtambua Mkaguzi wa FEMA

Release Date:
Oktoba 15, 2021

Wakaguzi wa FEMA hurekodi uharibifu uliosababishwa na mkasa. Hawatoi uamuzi ikiwa unastahili kupata msaada wa FEMA au kiasi cha pesa au hata aina ya msaada utakaotolewa na FEMA. Ni vizuri kuwajibu ikiwa watawasiliana nawe.  

Zifuatazo ni njia za kutambua ikiwa mtu anayekugongea mlango au kukupigia simu ni mkaguzi wa FEMA:

Ukaguzi wa moja kwa moja: Wafanyakazi na makandarasi wote wa FEMA huwa na vitambulisho rasmi.  Waombaji misaada wanapaswa kusisitiza kuona vitambulisho rasmi vya wakaguzi ambavyo huwa na picha na majina yao. Wakaguzi wenye kandarasi na FEMA watakuwa na vitambulisho vilivyotolewa na waajiri wao.  Vilevile, navyo vitakuwa na majina, picha, labda na nambari ya kitambulisho.

Ukaguzi kwa njia ya simu: Wakaguzi huhakikisha kuwa wamemfikia mwombaji halali kwa kumuuliza ataje nambari nne za mwisho katika nambari yake ya usajili ya FEMA yenye tarakimu tisa. Mkaguzi humsomea mwombaji tarakimu nne za mwanzo kwenye nambari ya usajili ya mwombaji. Waombaji hupata nambari za usajili baada ya kukamilisha maombi ya msaada wa FEMA.

Mambo mengine ya kufahamu kuhusu wakaguzi wa FEMA ni:

  • Hawaombi pesa ili kufanya ukaguzi na hawakupi hakikisho kwamba utapata pesa.
  • Japo wao huwa na anwani yako waliyotoa kwenye maombi yako ya msaada wa FEMA, lakini wanaweza kuwasiliana nawe kupata maelekezo ya jinsi ya kuifikia nyumba yako.
  • Wanawasiliana kwa kupiga simu, kutuma arafa na barua pepe—kutumia taarifa zako za mawasiliano ulizopeana kwenye maombi yako ya FEMA.
  • Wakaguzi wanaweza kupiga simu kutumia simu zilizotolewa na FEMA au zao za kibinafsi, na kodi za eneo (area codes) zinapopigiwa simu zaweza kuwa za nje ya Jimbo la New York.
  • Kuvaa shati au jaketi yenye nembo ya FEMA hakuwezi kuchukuliwa kama kitambulisho rasmi. Sisitiza uonyeshwe kitambuslisho chao cha FEMA chenye picha yao. Sheria za kitaifa zinakataza kupiga picha au kutoa nakala ya vitambulisho vya serikali ya Marekani. Ni kosa linaloadhibiwa kwa kulipa faini au kifungo cha jela.   
  • Ikiwa hauko nyumbani, mkaguzi atakuachia barua hapo nyumbani (mlangoni).

Ukirudi nyumbani na kukuta barua ya mkaguzo mlangoni pako, usiipuuze. Barua hiyo ni sehemu ya mchakato wa ukaguzi na itakuwa na jina na njia ya mawasiliano ya mkaguzi huyo. Ikiwa ulituma maombi kwa FEMA na ulikuwa unatarajia mkaguzi kukutembelea, wasiliana naye ili aendelee na mchakato wa ukaguzi. Usichapishe taarifa za mawasiliana za mkaguzi kwenye mitandao ya kijamii.

Ukipata barua ya mkaguzi mlangoni pako na hukuwa umetuma maombi ya msaada kwa FEMA, wasiliana na FEMA au Kitengo cha FEMA cha Uchunguzi wa Ulaghai na Ukaguzi kupitia 866-223-0814 au utume barua pepe kwa StopFEMAFraud@fema.dhs.gov. Mkaguzi wa FEMA alikuwa akifuata tu maelekezo na itifaki. Unaweza kuwasiliana na mkaguzi na kumweleza kwamba hukuomba msaada wa FEMA. Mkaguzi baadaye atapiga ripoti ya kilichojiri.

Unaweza kuthibitisha ikiwa una ukaguzi karibuni kwa kupiga Simu ya Usaidizi ya FEMA kupitia 800-621-3362 au kutumia huduma za video za relay (VRS). Aidha, waweza kutembelea DisasterAssistance.gov na kuchagua “Review Status.” Unashauriwa kuhakikisha kwamba anwani yako ni sahihi na kupeana maelekezo wazi jinsi ya kuifikia nyumba yako.

Ukihisi kwamba wewe au yeyote unayemjua amekuwa mwathiriwa wa ulaghai au wizi wa vitambulisho, piga ripoti mara moja katika kituo cha polisi kilicho karibu nawe au katika idara ya sherifu. Waweza pia kuwasiliana na Kitengo cha FEMA cha Uchunguzi wa Ulaghai na Ukaguzi kupitia kwa nambari za simu zilizotolewa hapo juu.

Kwa taarifa za hivi karibuni kuhusu juhudi za kutoa misaada kwa waathiriwa wa Kimbunga Ida, tembelea fema.gov/disaster/4615. Fuatilia taarifa zetu kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii kupitia twitter.com/femaregion2 na facebook.com/fema.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho