NEW YORK – Msaada wa nchi wa kukabiliana na majanga si wa wamiliki wa nyumba tu. Pia, unapatikana kwa wakodishaji wanaostahili, na unaweza kushughulikia gharama kama vile fanicha, vifaa vinahusiana na kazi, urekebishaji wa gari, na vilevile gharama za kitiba na za matibabu ya meno zinazosababishwa na janga.
Wakodishaji wanaoishi katika majimbo ya Bronx, Kings, Nassau, Queens, Richmond, Rockland, Suffolk na Westchester waliopata uharibifu, hasara au hawawezi kuishi katika nyumba zao baada ya Kimbunga cha Ida wanaweza kustahili kupata msaada kutoka kwa FEMA na Shirika la Marekani linalosimamia Biashara Ndogo.
Msaada wa FEMA wa kukodisha umenuiwa kushughulikia kodi ya kila mwezi na gharama za huduma muhimu (k.v., gesi, umeme na maji). Misaada ya FEMA pia inaweza kutumika kwa amana za usalama lakini si kwa simu, nyaya au huduma za intaneti.
Wakodishaji lazima waweze kudhibitisha kwamba waliishi katika makao yaliyoharibiwa na janga kabla ya kupokea msaada wa Makao ya FEMA na aina nyingine za Misaada ya Mahitaji Mengine ya FEMA (k.v., ya mali ya kibinafsi na gharama za kuhama na kuhifadhi).
Ili kudhibitisha kwamba aliishi katika nyumba hiyo, nusura anaweza kuwasilisha kwa FEMA: makubaliano ya kukodi au kuishi, risiti za kodi, gharama za huduma, stetimenti ya mfanyanyabiashara, stetimenti ya ofisa wa umma, kadi za utambulisho, stakabadhi za shirika la ruzuku ya jamii, stakabadhi za shule katika eneo, stakabadhi za udhamini wa nchi au jimbo, usajili wa gari, shuhuda ya mahali unapoishi au stakabadhi zingine za mahakamani na stakabadhi za kuegesha makao yanayoweza kuhamishwa. Wataalamu wa laini ya msaada ya FEMA ya 800-621-3362 (711/VRS) wanaweza kuandaa habari zaidi kuhusu stakabadhi zinazokubalika, tarehe zao na maelezo.
Wakodishaji wanaweza kutumwa kwenye shirika la Marekani linalosimamia Biashara Ndogo, ambalo huandaa mikopo ya janga yenye riba ya chini kwa manusura. Mikopo ya SBA inaweza kusaidia kulipia hasara zisizosimamiwa na bima. Wakodishaji wanaweza kuomba mikopo ya hadi dola 40,000 ili kurekebisha au kununua vitu vya nyumba vilivyoharibiwa kutia ndani mavazi, fanicha, vifaa na vitu vingine vya kibinafsi kutia ndani magari. Wale ambao hawastahili mikopo ya SBA wanaweza kurudishwa kwa programu ya msaada wa Mahitaji Mengine ya FEMA.
Ikiwa umetumwa kwa SBA, unapaswa kujaza na kuwasilisha ombi. Ikiwa ombi lako limekubaliwa, si lazima ukubali mkopo lakini kukosa kuwasilisha ombi kunaweza kukufanya usistahili kupata msaada mwingine wa FEMA ambao huenda ukapata.
Kuna njia kadhaa za kujiandikisha kwa ajilii ya msaada wa FEMA:
- Tembelea DisasterAssistance.gov, tumia programu ya FEMA ya simu ya mkononi au pigia laini ya Msaada ya FEMA ya 800-621-3362 (711/VRS). Laini zinatumika kati ya saa mbili asubuhi hadi saa moja jioni siku saba za wiki, na wahudumu wanaweza kukuunganisha na mtaalamu anayezungumza lugha yako. Ikiwa unatumia huduma ya kupeperusha kama vile huduma ya kupeperusha video, huduma za kutoa maelezo ya simu au zingine, wape FEMA namba ya huduma hiyo.
FEMA pia imefungua Vituo vya Kurejesha Hali Baada ya Janga ambapo unaweza kukutana uso kwa uso na wafanyakazi wa FEMA na wawakilishi wa mashirika mengine ya nchi na jimbo ambao wanaweza kuandaa habari kuhusu msaada wa janga unaoweza kuupata. Ili kupata kituo cha kurejesha hali kilicho karibu nawe, tembelea DRC Locator (fema.gov).
Ili kujaza ombi la mkopo wa SBA, tembelea tovuti salama ya SBA kwa https://DisasterLoanAssistance.sba.gov. Pia, unaweza kutuma barua pepe kwa DisasterCustomerService@SBA.gov au pigia Kituo cha Huduma za Wateja cha SBA kwa 800-659-2955 ili kupata habari zaidi.
Siku ya mwisho ya kujaza ombi la msaada wa FEMA ni Ijumaa, Nov. 5.
Kwa habari zaidi mtandaoni na vijitabu vinavyoweza kupakuliwa vya FEMA, tembelea DisasterAssistance.gov na ubonyeza “Information.”
Ili kutumwa kwa mashirika yanayotegemeza huduma hususa za jamii, wasiliana na kituo kilicho karibu zaidi na wewe cha 211Counts kwa https://www.211nys.org/contact-us au piga 211. Kwa waakazi wa Jiji la New York, piga 311.
Ili kupata habari za karibuni zaidi za New York kuhusu juhudi za kurejesha hali baada ya Kimbunga cha Ida, tembelea www.fema.gov/disaster/4615. Tufuate kwa Twitter kwa twitter.com/femaregion2 na www.facebook.com/fema.