Tumia Vizuri Ruzuku Yako ya FEMA

Release Date Release Number
009
Release Date:
Oktoba 4, 2021

NEW YORK—Wewe kama mwathiriwa stahiki wa mkasa uliyeanza kupokea fedha ya msaada wa kodi ya nyumba, matengenezo ya nyumba, au aina nyingine za usadidizi, unahakikishiwa kwamba fedha za mikasa hazina tozo lolote. Barua ya taarifa kutoka kwa FEMA itakuarifu kuhusu matumizi mwafaka ya fedha ya msaada wa mikasa. FEMA inakusihi utumie hizi fedha kama ilivyoelezwa katika barua ya taarifa na zitumike tu kugharamia mambo yanayohusiana na mkasa.

Hivi hapa ni vidokezo muhimu:

FEMA watakutumia barua ya kukuarifu kuhusu aina za misaada unazostahiki kupata na kiwango cha fedha za msaada kinachotolewa na FEMA kwa kila hitaji stahiki. Mahitaji haya ni pamoja na:

  • Matengenezo ya makazi (k.v. kuta na paa, maji, tangi na mfumo wa maji taka).
  • Usaidizi wa kulipa kodi sehemu nyingine kwa muda mfupi.  
  • Matengenezo au ununuzi wa gari la kimsingi lililoharibika katika mkasa.
  • Malipo ya kimatibabu ambayo hayajakatiwa bima kwa ajili ya majeraha yaliyotokana na mkasa.
  • Matengenezo au ununuzi wa zana/vifaa maalum vya kazi.
  • Vifaa muhimu vya kielemu (k.v. kompyuta, vitabu vya shule, na vifaa vingine).
  • Gharama za kuhama na kutunza vitu zinazotokana na mkasa na gharama nyingine zitokanazo na mkasa.

 

Unaweza kutumia ruzuku yako ya FEMA kwa ajili ya kufanya makazi yako yawe salama, safi, na yenye kukalika. Kumbuka kutunza kumbukumbu ya hesabu ya jinsi umetumia ruzuku yako ya mkasa na kutunza risiti zote angalau kwa kipindi cha miaka mitatu kama ithibati.  

Ruzuku za mikasa si za kugharamia matumizi ya kawaida ya kila siku kama vile bili za kawaida, chakula, matibabu ya kawaida au ya meno, ziara, burudani, au gharama nyingine ambazo hazihusiani na mkasa.    

Sheria za kitaifa zinakataza kuomba misaada kutoka vyanzo mbalimbali.

Unaweza kuomba msaada wa FEMA kupitia DisasterAssistance.gov, kutumia App ya simu ya FEMA au kupiga simu ya Huduma ya FEMA kupitia 800-621-3362 (711/VRS).  Laini za simu hufanya kazi kuanzia saa mbili asubuhi (8 a.m.) hadi saa moja jioni (7 p.m.) siku saba za wiki, na wahudumu wanaweza kukuunganisha na mtaalamu anayezungumza lugha yako. Ikiwa unatumia nambari au laini ya simu ya wasiosikia/walemavu (relay call) kama vile huduma ya relay ya video, huduma ya simu ya maandishi (captioned telephone) au huduma nyingine, wape FEMA nambari ya huduma hiyo.

Kupata rufaa au maelekezo kwenda kwa mashirika yanayoshughulikia mahitaji ya jamii mahususi, wasiliana na kituo cha 211 kilicho karibu nawe kupitia https://www.211nys.org/contact-us. Ukiwa katika Jiji la New York, piga simu 311. Kwa maeneo ya nje ya Jiji, piga simu 211.

Kwa taarifa rasmi kuhusu juhudi na shughuli za uokoaji baada ya kimbunga, tafadhali tembelea https://www.fema.gov/disaster/4615. Fuatilia taarifa zetu kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii kupitia twitter.com/femaregion2 na www.facebook.com/fema.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho