Wamiliki wa nyumba na wapangaji wa Vermont katika kaunti za Caledonia, Chittenden, Lamoille, Orange, Orleans, Rutland, Washington, Windham na Windsor ambao waliathiriwa na dhoruba kali, mafuriko, maporomoko ya ardhi na maporomoko ya udongo yaliyotokea kuanzia Julai 7, 2023, na kuendelea wanaweza kustahili ufadhili wa FEMA kwa ajili ya hasara ya mali ya kibinafsi na gharama zingine zinazostahili.
Mpango wa Watu Binafsi na Familia
Mpango wa Watu Binafsi na Familia ya FEMA (IHP) Huandaa msaada kwa watu binafsi na familia zinazostahili ambazo hazina bima au bima haitoshi kugharamia mahitaji makubwa kutokana na dhoruba kali za Julai, mafuriko, maporomoko ya ardhi na maporomoko ya udongo. Hii inajumuisha misaada zaidi ya kurekebisha nyumba.
Kiasi na aina ya msaada huamuliwa na gharama zako, na zinaweza kujumuisha:
- Msaada wa Matibabu na Matibabu ya Meno
- Msaada wa Kutunza Mtoto
- Msaada wa Vitu vidogo vidogo
- Msaada wa Kuhama na Kuhifadhi
- Msaada wa Mazishi
Aina nyingine za misaada zinapatikana tu ikiwa mwombaji atatuma maombi ya mkopo wa majanga kutoka kwa Usimamizi wa Biashara Ndogo ya Marekani (SBA), na hastahili. Kukamilisha ombi haimaanishi kuwa lazima ukubali mkopo. Msaada wa ziada unaoweza kupatikana unajumuisha:
- Msaada wa Mali Binafsi
- Msaada wa Usafiri
- Sera ya Kikundi cha Bima ya Mafuriko (GFIP)
Zungumza na mtaalamu wa FEMA ili upate maelezo zaidi. Wataalamu wa FEMA wanapatikana kwa simu kwa 800-621-3362 au ana kwa ana katika Vituo vya Msaada wa Majanga. Ili kupata kituo cha karibu zaidi, tembelea fema.gov/drc.
Matakwa ya Jumla ya Mpango
Kwa ujumla, wanaotuma maombi lazima wakidhi masharti yote yafuatayo ili kutuma maombi:
- Wewe au mtu anayeishi nawe ni raia wa Marekani, mwananchi asiye raia, au mgeni anayestahili.
- Umepita utambulisho wa FEMA na uthibitisho wa makazi
- Lazima upite uthibitishaji wa umiliki ili kupata Msaada wa Kurekebisha na Kubadilisha Nyumba.
- Nyumba yako ya msingi iko katika eneo la majanga lililoteuliwa na rais na hauwezi kuishi au kuifikia.
- Huna bima, au uliwasilisha dai la bima na haishughulikii hasara zako zote.
Tuma Maombi ya Msaada wa FEMA
Tuma maombi mtandaoni katika DisasterAssistance.gov, pakua FEMA mobile app kwa simu ya mkononi, au piga simu kwa laini ya msaada bila malipo kwa 800-621-3362. Tafsiri ya lugha inapatikana. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji kama vile huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari ya huduma hiyo unapotuma ombi.
Kupata video ya jinsi ya kutuma maombi ya usaidizi, nenda kwa FEMA Accessible: Three Ways to Register for FEMA Disaster Assistance - YouTube.
Kupata habari ya hivi karibuni zaidi fema.gov/disaster/4720. Fuata akaunti ya FEMA Region 1 katika Twitter twitter.com/FEMARegion1 au Ukurasa wa Facebook ya FEMA katika facebook.com/FEMA.
Kupata masasisho kuhusu shughuli za msaada za Vermont, fuata Wakala wa Usimamizi wa Dharura wa Vermont twitter.com/vemvt kwenye Twitter au Facebook facebook.com/VermontEmergencyManagement.
FEMA imejitolea kuhakikisha msaada wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza, au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa maafa au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi kuwa ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wanaotumia lugha nyingi wanapatikana.