Vermont Dhoruba Kali, Mafuriko Na Maporomoko Ya Ardhi.
Kipindi cha Tukio: Jul 7, 2023 - Jul 17, 2023
Tarehe ya Kutangaza: Jul 14, 2023
Viunganishi vya Haraka
- Rasilimali za urejeshaji: Jimbo na Mitaa | Kitaifa
- Wasiliana: Mitandao ya Kijamii | Programu ya Simu na Ujumbe
- Ushauri masaa 24/7: Nambari ya Msaada ya Majanga
Kwenye Ukurasa Huu
Mengi zaidi Kuhusu Janga Hili
Msaada kwa Watu Binafsi na Familia Baada ya Majanga
Ikiwa una bima, unapaswa kuwasilisha dai kwa kampuni yako ya bima mara moja. Msaada wa FEMA hauwezi kusaidia na hasara ambazo tayari zimelipwa na bima
Tuma Maombi ya Msaada wa Majanga
Njia ya haraka zaidi ya kutuma ombi ni kupitia DisasterAssistance.gov. Unaweza pia kutuma maombi kupitia FEMA mobile app au kwa kupiga Simu kwa laini ya Msaada ya FEMA kwa 800-621-3362. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji video, huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi, au huduma zingine za mawasiliano, tafadhali pea FEMA nambari mahususi uliyokabidhiwa kwa huduma hiyo.
Pata maelezo zaidi kuhusu mchakato wa kutuma maombi
Pata Msaada wa Haraka
Tafuta usaidizi wa mahitaji ambayo FEMA haijaidhinishwa kutoa. Wasiliana na maafisa wa usimamizi wa dharura wa eneo lako, mashirika ya hiari au kwa kupiga 2-1-1 ya eneo lako. Laini ya Msaada ya FEMA (800-621-3362) inaweza kutoa marejeleo ya ziada. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji video, huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi, au huduma zingine za mawasiliano, tafadhali pea FEMA nambari mahususi uliyokabidhiwa kwa huduma hiyo.
Niliambiwa Nipigie simu Usimamizi wa Biashara Ndogo ya Marekani
FEMA hairuhusiwi kutoa msaada wa majanga kwa hasara fulani zinazolipwa na mikopo ya majanga inayotolewa na Usimamizi wa Biashara Ndogo ya Marekani (SBA). SBA hutoa mikopo ya majanga yenye riba nafuu kwa watu binafsi na familia ili kusaidia na hasara za majanga. FEMA hushirikiana na SBA kubaini kama unaweza kustahili kupata Msaada wa Mali ya Kibinafsi, Msaada wa Usafiri, au Sera ya Kikundi ya Bima ya Mafuriko.
FEMA itakuelekeza kwa SBA moja kwa moja ili uzingatiwe kwa mkopo wa majanga ikiwa unatimiza viwango vya mapato vya SBA. FEMA hutumia mapato ya jumla ya mwaka ya familia yako na idadi ya wanaoitegemea ili kubaini kama unapaswa kutumwa kwa SBA.
Ukielekezwa kwa SBA, FEMA itawasiliana nawe kupitia mfumo wa kipiga simu kiotomatiki ili kueleza jinsi ya kutuma maombi ya mkopo wa majanga. Ni lazima ukamilishe na urudishe ombi la mkopo ili kuzingatiwa kwa mkopo wa SBA au aina fulani za msaada wa FEMA. Si lazima ukubali ofa ya mkopo ya SBA. Hata hivyo, ikiwa umeidhinishwa kupokea mkopo wa SBA, na hukuukubali, hutarejeshwa kwa FEMA kwa msaada wa mali binafsi au usafiri.
Kwa maelezo zaidi kuhusu mpango wa mkopo wa majanga ya SBA, tafadhali piga simu kwa SBA kwa 800-659-2955 (TTY: 800-877-8339). Maelezo ya SBA pia yanapatikana katika www.SBA.gov/disaster au kwa barua pepe kwa disastercustomerservice@sba.gov.
Pata maelezo zaidi kuhusu mikopo ya SBA
Nilituma maombi ya Msaada. Nini Kinachofuata?
Kama Una Bima
Tafadhali wasiliana na kampuni yako ya bima haraka iwezekanavyo ili kuwasilisha dai. FEMA inaweza tu kutoa pesa baada ya kupata malipo ya bima yako. Ikiwa bima yako haishughulikii gharama zako zote za ukarabati wa nyumba au ujenzi upya, FEMA inaweza kukusaidia.
FEMA haiwezi kutoa pesa kwa gharama zinazoshughulikiwa na bima au udhamini mara mbili kutoka kwa chanzo kingine. Unapopata malipo yako ya bima au kunyimwa, tafadhali tuma nakala kwa FEMA haraka uwezavyo.
Ikiwa malipo yako ya bima yatacheleweshwa zaidi ya siku 30 kutoka wakati unapowasilisha dai lako, piga Simu kwa laini ya msaada ya FEMA kwa 800-621-3362.
Pata maelezo zaidi kuhusu hatua baada ya kutuma ombi
Ikiwa hauna Bima
FEMA itathibitisha hasara ulizopata kutokana na majanga. Shirika litapanga muda wa kukagua nyumba yako ikiwa uliripoti uharibifu wa nyumba yako au mali ya kibinafsi. Au FEMA itakuomba utume hati ili kuthibitisha gharama zako.
Utapokea barua za arifa kutoka kwa FEMA kupitia barua au barua pepe zinazoelezea hatua zako zinazofuata. Ikihitajika kulingana na hasara ulizoripoti, mkaguzi atawasiliana nawe kwa simu ili kupanga ukaguzi. Ukikosa kupatikana kwa simu, wataacha ujumbe wa sauti na kufanya majaribio mengi ya kuwasiliana nawe. Mkaguzi hapaswi kuhitaji kutazama risiti za ukarabati au picha za uharibifu. Lakini ukianza kusafisha kabla ya ukaguzi, FEMA inapendekeza upige picha, uandike orodha ya hasara ulizopata, na uhifadhi risiti za gharama zako zote zilizosababishwa na majanga.
Broshua ya "Msaada Baada ya Majanga".
Ikitafsiriwa katika lugha 27, broshua ya "Msaada Baada ya Majanga" ni chombo ambacho kinaweza kushirikiwa katika jamii yako ili kuwasaidia watu kuelewa aina za usaidizi wa FEMA ambao unaweza kupatikana ili kusaidia watu binafsi na familia katika kurejea maisha baada ya majanga.
Kustahili Uraia na FEMA
FEMA imejitolea kusaidia manusura wote wanaostahili kupata nafuu, wakiwemo raia wa Marekani, wakazi wasio raia na wageni wanaostahili. Pata maelezo zaidi kuhusu Matakwa ya Hali ya Uraia na Uhamiaji kwa manufaa ya serikali ya umma.
Tafuta Mshauri wa Makazi
Idara ya Makazi na Maendeleo ya Miji ya Marekani (HUD) hutoa usaidizi kwa mtandao wa kitaifa wa mashirika ya ushauri wa nyumba (HCAs) na washauri walioidhinishwa. HCA zinazoshiriki katika HUD zimeidhinishwa na kufunzwa kutoa zana kwa wamiliki wa nyumba wa sasa na watarajiwa na wapangaji ili waweze kufanya maamuzi mazuri kushughulikia mahitaji yao ya makazi kulingana na hali zao za kifedha.
Kuthibitisha Umiliki wa Nyumba au Ukaaji
FEMA inahitaji kuthibitisha kuwa uliishi katika anwani iliyo katika ombi lako kama makazi yako ya msingi kabla ya kutoa aina nyingi za usaidizi. FEMA pia inahitajika kuthibitisha kuwa unamiliki nyumba yako kabla ya kutoa msaada wa ukarabati wa nyumba au kubadilisha nyumba. Jifunze zaidi kuhusu mchakato huu.
Kama sehemu ya juhudi zetu za kufanya mchakato wa msaada wa majanga kuwa mwepesi na kupunguza mzigo kwa waombaji, tunajaribu kuthibitisha umiliki na ukaaji kwa kutumia utafutaji wa rekodi za umma kiotomatiki.
Iwapo hatuwezi kuthibitisha kuwa uliishi au kumiliki nyumba uliyoorodhesha kwenye ombi lako, tutakuomba utupe hati za kuthibitisha umiliki na/au ukaaji ili utusaidie kubainisha ikiwa umeidhinishwa kupokea msaada.
Je, Nitakata Vipi Rufaa Dhidi ya Uamuzi huo?
Ukipokea barua inayosema kwamba hujaidhinishwa kupokea msaada au kwamba ombi lako halijakamilika, bado unaweza kukamilisha ombi au kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo ndani ya siku 60 baada ya kupokea barua ya uamuzi. Barua inaweza kutumwa kwako au kuwekwa kwenye akaunti yako ya Kituo cha Msaada wa Majanga ikiwa umefungua akaunti.
Pata maelezo zaidi kuhusu rufaa
Maswali Yanayoulizwa Mara Kwa Mara na Uvumi
Pata maelezo zaidi kuhusu uvumi unaohusiana na majanga na jinsi ya kuripoti ulaghai. Unaweza pia kupata majibu kwa maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu makazi ya dharura, usaidizi wa majanga, bima ya mafuriko na zaidi.
Rasilimali katika Lugha nyingi
Unaweza kupata picha za mitandao ya kijamii zenye ujumbe muhimu wa usalama katika lugha mbalimbali, ikijumuisha Kiingereza, Kichina, Kihispania na Kivietinamu.
Pia tuna video katika Lugha ya Ishara ya Marekani (ASL) kuhusu mada zinazojumuisha:
Rasilimali za Mitaani
Habari za Mitaani
Habari za Nchini na Vyombo vya Habari
Tembelea ukurasa wa Habari na Vyombo vya Habari kwa matukio, karatasi za ukweli, taarifa kwa vyombo vya habari na njia zingine za mawasiliano.
Jinsi ya Kusaidia
Kujitolea na Kutoa Michango
Kurejesha kunaweza kuchukua miaka mingi baada ya janga. Kuna njia nyingi za kusaidia kama vile kutoa pesa taslimu, vitu vinavyohitajika au wakati wako. Jifunze zaidi kuhusu jinsi ya kuwasaidia wale wanaohitaji.
Usijitume kwenye maeneo ya majanga. Mashirika yanayoaminika katika maeneo yaliyoathiriwa yanajua mahali watu wa kujitolea wanahitajika. Fanya kazi na shirika linaloaminika ili kuhakikisha kuwa una usalama, mafunzo na ujuzi ufaao unaohitajika ili kujitolea.
Wakala wa Ushirikiano wa Kujitolea wa FEMA (VALs) hujenga uhusiano na kuratibu juhudi na mashirika ya hiari, ya kidini na ya kijamii yanayojishughulisha na majanga.
Kufanya Biashara na FEMA
Iwapo ungependa kutoa huduma na bidhaa zinazolipiwa kwa ajili ya usaidizi wa majanga, tembelea ukurasa wetu wa Kufanya Biashara na FEMA ili kuanza.
Ikiwa unamiliki biashara inayohusika na uondoaji wa vifusi na ungependa kufanya kazi ya kusafisha maeneo yaliyoathirika, tafadhali wasiliana na serikali ya mtaa katika maeneo yaliyoathirika ili kutoa huduma zako.
Majukumu ya Ufadhili
Usaidizi wa Mtu Binafsi | Kiasi |
---|---|
Jumla ya Msaada wa Makao (HA) - Dola Zilizoidhinishwa | $18,393,573.90 |
Jumla ya Msaada wa Mahitaji Mengine (ONA) - Dola Zilizoidhinishwa | $1,591,527.61 |
Jumla ya Dola za Mpango wa Mtu Binafsi na Familia Zilizoidhinishwa | $19,985,101.51 |
Maombi ya Msaada wa Mtu Binafsi Yameidhinishwa | 3250 |
Msaada wa Umma | Kiasi |
---|---|
Total Public Assistance Grants Dollars Obligated | $79,677.25 |
Orodha ya Vituo vya Msaada wa Majanga (DRC)
Vituo vya Msaada wa Majanga huwapa waathirika wa majanga taarifa kutoka kwa FEMA na Usimamizi wa Biashara Ndogo za Marekani. Manusura wa majanga wanaweza kupata usaidizi wa kutuma maombi ya usaidizi wa serikali, kujifunza kuhusu aina za msaada unaopatikana, kujifunza kuhusu mchakato wa kukata rufaa na kupata masasisho kuhusu maombi.
Ludlow Community Center
Anwani
37 Main St
Ludlow, Vermont 05149
Windsor
Get Directions
Masaa ya DRC
Jumatatu: | 8:00 AM - 6:00 PM |
Jumanne: | 8:00 AM - 6:00 PM |
Jumatano: | 8:00 AM - 6:00 PM |
Alhamisi: | 8:00 AM - 6:00 PM |
Ijumaa: | 8:00 AM - 6:00 PM |
Jumamosi: | 9:00 AM - 2:00 PM |
Jumapili: | IMEFUNGWA |
MAELEZO
Soft Opening Hours of Operation 9/19 1:00 - 6:00PM.
Barre Auditorium
Anwani
16 Auditorium Hill
Barre, Vermont 05641
Washington
Get Directions
Masaa ya DRC
Jumatatu: | 8:00 AM - 6:00 PM |
Jumanne: | 8:00 AM - 6:00 PM |
Jumatano: | 8:00 AM - 6:00 PM |
Alhamisi: | 8:00 AM - 6:00 PM |
Ijumaa: | 8:00 AM - 6:00 PM |
Jumamosi: | 9:00 AM - 2:00 PM |
Jumapili: | IMEFUNGWA |
MAELEZO
Soft opening on 7/26 @1PM.
Waterbury Armory
Anwani
294 Armory Drive
Waterbury, Vermont 05676
Washington
Get Directions
Masaa ya DRC
Jumatatu: | 8:00 AM - 6:00 PM |
Jumanne: | 8:00 AM - 6:00 PM |
Jumatano: | 8:00 AM - 6:00 PM |
Alhamisi: | 8:00 AM - 6:00 PM |
Ijumaa: | 8:00 AM - 6:00 PM |
Jumamosi: | 9:00 AM - 2:00 PM |
Jumapili: | IMEFUNGWA |
MAELEZO
Soft Opening on 7/21 at 1PM.