Kile Wakazi wa Vermont Wanahitaji Kujua Kuhusu Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Mafuriko

Release Date:
Agosti 10, 2023

Dhoruba za hivi majuzi za Vermont zinaonyesha kiasi cha uharibifu ambayo mafuriko yanaweza kusababisha. Kulinda nyumba au biashara yako kutumia sera kutoka kwa Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Mafuriko kunaweza kukusaidia kujiandaa kwa ajili ya - na shughuli za urejesho baada ya - mafuriko wakati ujao.

Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Mafuriko ni nini?

Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Mafuriko husaidia watu katika maeneo yaliyo katika hatari kubwa ya mafuriko kupata bima. Inasimamiwa na FEMA na kuwasilishwa na mtandao wa zaidi ya kampuni 50 za bima, NFIP hutoa bima ya mafuriko kwa wamiliki wa mali, wapangaji na wafanyabiashara ili kuwasaidia kurejea haraka maji ya mafuriko yanapopungua.

Kwa Wapangaji, Wamiliki wa Nyumba na Biashara

Sera za NFIP zinapatikana kwa wapangaji, wamiliki wa nyumba na biashara katika maeneo ambayo yanashiriki katika mpango. Jamii zinazoshiriki katika NFIP hufuata mpango wa kupunguza uharibifu wa mafuriko, ambao unaweza kujumuisha kuwahitaji wajenzi kuweka baadhi ya hatua za ulinzi au kuzuia maendeleo katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko zaidi. Ili kuona kama jamii yako inahudumiwa, piga simu kwa Kituo cha Simu za Rufaa cha NFIP kwa 800-427-4661 au tembelea FloodReady.Vermont.gov/Find_Funding/Flood_Insurance.

Kwa nini ninahitaji bima ya mafuriko?

Hata kama huishi katika eneo la "hatari kubwa", nyumba yako bado inaweza kupatwa na mafuriko - zaidi ya asilimia 20 ya madai ya NFIP yanatoka nje ya maeneo yenye hatari zaidi. Inchi moja tu ya maji ya mafuriko yanaweza kusababisha uharibifu wa hadi $25,000. Msaada wa FEMA utafanya nyumba yako kuwa salama baada ya mafuriko, lakini hauwezi kushughulikia uharibifu wote. Chanzo kikubwa cha fedha za msaada baada ya majanga ni bima.

Bima ya Wamiliki wa Nyumba sio Bima ya Mafuriko

Sera nyingi za bima za wamiliki wa nyumba na wapangaji hazishughulikii uharibifu wa mafuriko. Ikiwa sera yako haijumuishi mafuriko kihususa, utahitaji bima tofauti ya mafuriko ili kushughulikiwa.

Nyumba yangu imefurika tu. Je, ninaweza kupata bima?

Haijalishi ni mara ngapi nyumba yako, fleti au biashara imefurika. Ikiwa jamii yako inashiriki katika NFIP, unastahili bima ya mafuriko.

Ikiwa una bima, tuma dai haraka iwezekanavyo. Pigia simu wakala wako, piga picha za uharibifu uliopata, na uhifadhi risiti za marekebisho yote. Kwa habari zaidi, tembelea www.FloodSmart.gov/How-Do-I-Start-My-Flood-Claim.

Ingawa kupata bima sasa hakutashughulikia uharibifu ambao tayari umetokea, kunaweza kukulinda kutokana na dhoruba zijazo. Unaweza kununua bima ya mafuriko wakati wowote. Sera nyingi zina muda wa kusubiri wa siku 30 baada ya kulipa malipo kabla ya sera kuanza kutumika.

Ikiwa umepata uharibifu wa mafuriko, FEMA inaweza kukusaidia. Ikiwa una bima, huhitaji kusubiri dai lako lichakatwe. Ili kutuma ombi, tembelea DisasterAssistance.gov, pakua FEMA App au piga simu kwa nambari ya usaidizi 800-621-3362. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji kama vile huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo unapotuma ombi.

Kupata msaada ana kwa ana, tembelea Kituo cha Msaada wa Majanga, ambapo wataalamu wa FEMA wanaweza kukusaidia kutuma maombi, kujibu maswali na kutoa marejeleo ya rasilimali. Ili kupata kituo karibu nawe, tembelea fema.gov/drc.

FEMA imejitolea kuhakikisha msaada wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa majanga au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi kuwa ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wanaozungumza lugha nyingi wanapatikana.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho