Kituo cha Kutoa Misaada ya Mikasa cha Kaunti ya kitafungwa kabisa Jumamosi saa kumi na mbili jioni (6 p.m.) japo wakazi walioathiriwa na Kimbunga Ida wanaweza kupata usaidizi wa maombi yao ufadhili wa mikasa. Usaidizi waweza kupatikana kwa njia ya simu, na mtandaoni.
Kituo hiki cha kutoa usaidizi kinapatikana Rose Caracappa Senior Center, 739 NY-25A eneo la Mount Sinai. Ijapokuwa hiki ndicho kituo cha pekee katika Kaunti ya Suffolk, Vituo vingine saba vya Kutoa msaada katika kaunti jirani vitaendelea kufanya kazi kuanzia saa 4 asubuhi (10 a.m.) hadi saa 12 jioni (6 p.m.) Ijumaa hadi Jumamosi. Vituo vyote vinafungwa siku za Jumapili. Hivi vituo ni:
-
- Hostos College, 450 Grand Concourse, Bronx, NY 10451
- Public Library, 136 Prospect Ave., Mamaroneck, NY 10543
- Queens College, 152-45 Melbourne Ave., Queens, NY 11367
- Medgar Evers College, 231 Crown St., Brooklyn, NY 11225
- College of Staten Island, 2800 Victory Blvd., Staten Island, NY 10314
- Michael J. Tully Park Physical Activity Center, 1801 Evergreen Ave., New Hyde Park, NY 11040
- Orangetown Soccer Club Complex, 175 Old Orangeburg Road, Orangeburg, NY 10962
Wataalamu wapo vituoni kujibu maswali yako yakiwemo maswali kuhusu kuchelewa kupokelewa kwa majibu kutoka kwa FEMA kuhusu ustahiki wako wa kupata ufadhili na kukusaidia kupakia stakabadhi zako kwenye akaunti yako.
Unaweza pia kutembelea Kituo chochote cha Kutoa Misaada na kukutana na wafanyakazi wa FEMA na wawakilishi wa mashirika mengine ya kitaifa na jimbo. Vituo hivi vilevile vinatumia teknolojia kuwasaidia walio na ulemavu. Ikiwa utahitaji mitambo maalum ya kiteknolojia, mwarifu mtaalamu unapopiga simu ya usaidizi ya FEMA.
Kutuma maombi ya ufadhili wa FEMA, tembelea DisasterAssistance.gov, piga Simu ya FEMA ya Usaidizi 800-621-3362, au utumie app ya FEMA kwenye simu. Ikiwa unatumia huduma ya relay ya video, huduma ya simu ya maandishi (captioned telephone) au huduma nyingine, wape FEMA nambari ya huduma hiyo. Wahudumu katika laini za usaidizi wanapatikana kuanzia saa 2 asubuhi (8 a.m.) hadi saa 1 jioni (7 p.m.) kila siku. Bonyeza 2 kupata huduma kwa lugha ya Kihispania au 3 kupata mkalimani anayezungumza lugha yako.
Waathiriwa hawalazimiki kutembelea Kituo cha Misaada ili waweze kusaidiwa. Ikiwa unaishi katika Kaunti za Bronx, Dutchess, Kings, Nassau, Queens, Richmond, Rockland, Suffolk au Westchester, na nyumba yako iliharibiwa, hasara ilitokea, au huwezi kuishi katika nyumba hiyo kutokana na athari za moja kwa moja za Kimbunga Ida, unahimizwa kutuma maombi ya ufadhili wa FEMA kabla ya kutembelea kituo cha ufadhili.
Makataa ya kutuma maombi ya ufadhili wa mikasa wa FEMA ni Jumatatu, Disemba 6.
Kupata habari zaidi mtandaoni pamoja na vijitabu vya FEMA vinavyoweza kupakuliwa, tembelea DisasterAssistance.gov kisha ubofye “Information.”
Kwa rufaa kwenda kwa mashirika yanayosaidia katika mahitaji mahususi ya jamii, piga simu 211 au temebelea https://www.211nys.org/contact-us. Kwa wakazi wa jiji la New York, piga simu 311.
Kwa taarifa za hivi karibuni kuhusu juhudi za kutoa misaada kwa waathiriwa wa Kimbunga Ida jijini New York, tembelea fema.gov/disaster/4615. Fuatilia taarifa zetu kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii kupitia twitter.com/femaregion2 na facebook.com/fema.