Kituo cha Msaada wa Majanga cha FEMA Kinafunguliwa katika Kaunti ya Lamoille na Caledonia

Release Date Release Number
022
Release Date:
Agosti 9, 2023

Vituo vya Kuokoa Majanga vitafunguliwa saa mbili asubuhi (8 a.m) Agosti 10 huko Johnson (Kaunti ya Lamoille) na Danville (Kaunti ya Caledonia) ili kuwasaidia wakazi wa Vermont walioathiriwa na dhoruba kali za Julai, mafuriko, maporomoko ya ardhi na maporomoko ya udongo. Kituo cha pamoja cha msaada, kituo cha muda kilichoanzishwa kwa ushirikiano kati ya mji, jimbo la Vermont na FEMA, kitasaidia manusura kutuma maombi ya usaidizi wa FEMA, kupakia hati na kujibu maswali ana kwa ana.

Masaa ya kawaida ya vituo vyote ni saa mbili asubuhi  (8 a.m) hadi saa moja jioni (7 p.m.) siku 7 kwa wiki.

Kituo cha Kaunti ya Lamoille kinapatikana katika:

Northern VT University -- McClelland Hall

131 College Hill Road

Johnson, VT 05656

Kituo cha Kaunti ya Caledonia kinapatikana katika:

Danville School

148 Peacham Road

Danville, VT 05828

Vituo vingine tayari vimefunguliwa katika:

Waterbury Armory
294 Armory Drive
Waterbury, VT 05676

ASA Bloomer Building
88 Merchants Row, Suite 330
Rutland, VT 05701

Barre Auditorium
16 Auditorium Hill
Barre, VT 05641

Barton Memorial Building
17 Village Square 
Barton, VT 05822

Springfield Health Center

100 River St. 

Springfield, VT 05156

  • Kituo cha Springfield kitafungwa kwa muda saa kumi na moja jioni  (5 p.m) Agosti 10; itafunguliwa tena saa saba  mchana (1 p.m.) Agosti 12.

Jamaica Fire Department 

4017 VT-30
Jamaica, VT 05343

FEMA huhamisha Vituo vya Msaada wa Majanga kulingana na mahali vinapohitajika zaidi. FEMA hufanya kazi kwa karibu na washirika wa jimbo na manispaa katika kubainisha maeneo hayo. Mara tu eneo linapoanza kuwa na kiasi kidogo cha ziara za usajili, FEMA na jimbo huratibu maeneo mapya ambapo kituo kinaweza kupokea ziara zaidi kutoka kwa wale wanaohitaji usaidizi.

Vituo vyote vinaweza kufikiwa na watu wenye ulemavu na mahitaji ya kutenda, na vina vifaa vya teknolojia ya usaidizi. Ikiwa unahitaji makao ya kuridhisha au mkalimani wa lugha ya ishara, tafadhali piga simu kwa 833-285-7448 (bonyeza 2 kwa Kihispania).

Wawakilishi kutoka Usimamizi wa Biashara Ndogo za Marekani (SBA) pia watakuwa kituoni kueleza jinsi ya kutuma maombi ya mikopo ya majanga yenye riba nafuu ya SBA kwa wamiliki wa nyumba, wapangaji, biashara na mashirika yasiyo ya kibiashara ya kibinafsi, na kutoa maelezo kuhusu kujenga upya ili kufanya nyumba zistahimili majanga zaidi.

Huhitaji kutembelea DRC ili kutuma maombi ya msaada wa FEMA. Kutuma ombi bila kutembelea kituo, piga simu kwa nambari ya msaada ya FEMA kwa 800-621-3362, nenda mtandaoni kwenye DisasterAssistance.gov au upakue FEMA App. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji kama vile huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo unapotuma ombi. Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ya msaada wa serikali ni Septemba 12, 2023.

FEMA imejitolea kuhakikisha msaada wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa majanga au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi kuwa ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wa lugha mbali mbali wanapatikana.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho