Mnamo Ijumaa, tarehe 14 Julai, 2023, Rais Joseph Biden alitangaza Maafa Makubwa katika jimbo la Vermont kutokana na dhoruba kali na mafuriko yaliyotokea tarehe 7 Julai, 2023 na kuendelea.
Wamiliki wa nyumba na wapangaji wa Vermont walioathiriwa na mafuriko ya hivi majuzi ambao wanaishi katika kaunti zilizoteuliwa hivi majuzi kupata Usaidizi wa Mtu Binafsi wanaweza kustahiki msaada kutoka FEMA.
Tangazo hili linawezesha ufadhili wa shirikisho kupatikana kwa watu walioathiriwa katika kaunti za Chittenden, Lamoille, Rutland, Washington, Windham na Windsor.
kaunti za ziada zinaweza kuongezwa baadaye kama inavyothibitishwa na matokeo ya tathmini zaidi za uharibifu.
Ikiwa una bima ya wamiliki wa nyumba au wapangaji, unapaswa kuwasilisha madai haraka iwezekanavyo. Kisheria, FEMA haiwezi kurudufisha faida kwa hasara zinazolipwa na bima. Ikiwa huna bima au una bima ya thamani ya chini, unaweza kustahiki usaidizi wa shirikisho.
Njia ya haraka na rahisi zaidi ya kutuma ombi ni kutembelea disasterassistance.gov au kupakua programu ya simu ya FEMA (pia katika Kihispania), popote unapofikia programu zako za simu.
Ikiwa haiwezekani kutuma ombi mtandaoni, piga simu 800-621-3362 (TTY: 800-462-7585). Nambari za simu za bila malipo zinafanya kazi kuanzia saa moja asubuhi hadi saa tano usiku (7 a.m. to 11 p.m.) EDT, siku saba kwa wiki, huku huduma za tafsiri za lugha zikipatikana.
Unapotuma ombi la usaidizi, hakikisha una taarifa zifuatazo:
- Nambari ya simu ya sasa ambapo unaweza kuwasiliana
- Anwani yako wakati wa maafa na anwani unamoishi sasa
- Nambari yako ya ruzuku ya kijamii ikiwa inapatikana
- Orodha ya jumla ya uharibifu na hasara
- Ikiwa una bima, nambari ya sera au wakala na/au jina la kampuni
Mara baada ya kuwa salama kufanya hivyo, anza kufanya usafi Piga picha ili kuweka kumbukumbu ya uharibifu kisha uanze kufanya usafi na kukarabati ili kuzuia uharibifu zaidi. Kumbuka kuhifadhi risiti kutoka kwa ununuzi wote unaohusiana na usafishaji na ukarabati.
Usaidizi wa maafa unaweza kujumuisha usaidizi wa kifedha kwa makazi ya muda na ukarabati wa nyumba pamoja na mipango mingine ya kusaidia familia kupata nafuu kutokana na athari za tukio hilo.
Mikopo ya maafa yenye riba nafuu ya U.S. Small Business Administration (Utawala wa Biashara Ndogo wa Marekani, SBA) inapatikana kwa wamiliki wa nyumba, wapangaji, biashara zenye ukubwa wowote na mashirika mengi yasiyotengeneza faida. Sawa na FEMA, SBA haiwezi kurudufisha faida kwa hasara zinazolipwa na bima.
Biashara zenye ukubwa wowote, wamiliki wa nyumba, wapangaji na mashirika yasiyotengeneza faida yanaweza kutuma ombi mtandaoni kwenye disasterloanassistance.sba.gov Kwa maswali na usaidizi wa kukamilisha ombi, piga simu 800-659-2955 au tuma barua pepe kwenda disastercustomerservice@sba.gov. SBA itajibu maswali mahususi kuhusu jinsi mkopo wa maafa unaweza kumsaidia kila aliyenusurika kupata nafuu kutokana na uharibifu wa maafa.
Kwa taarifa za hivi karibuni tembelea fema.gov/disaster/4720. Fuata akaunti ya FEMA Region 1 kwenye Twitter twitter.com/FEMARegion1 au ukurasa wa Facebook kwenye facebook.com/FEMARegion1.
Kwa taarifa za hivi karibuni kuhusu uitikiaji na uokoaji wa Vermont, fuata Vermont Emergency Management Agency twitter.com/vemvt kwenye Twitter na Facebook facebook.com/vermontemergencymanagement.
Ufadhili wa shirikisho pia unapatikana kwa jimbo, kabila na serikali za mitaa zinazostahiki na mashirika fulani ya kibinafsi yasiyotengeneza faida kwa msingi wa kugawana gharama kwa ajili ya hatua za ulinzi wa dharura. Ufadhili unapatikana katika kaunti za Addison, Bennington, Caledonia, Chittenden, Essex, Franklin, Grand Isle, Lamoille, Orange, Orleans, Rutland, Washington, Windham na Windsor counties kwa hatua za dharura za ulinzi.
Kaunti zote katika Jimbo la Vermont zinastahiki kutuma maombi ya usaidizi chini ya Hazard Mitigation Grant Program (Mpango wa Ruzuku ya Kupunguza Hatari).