Siku Tatu Zimesalia kwa Wakazi wa Missouri Kuomba Usaidizi wa Kibinafsi wa FEMA

Release Date Release Number
26
Release Date:
Novemba 4, 2022

Watu walioathiriwa moja kwa moja na dhoruba kali za Julai 25-28 na mafuriko katika jiji la Saint Louis na Kaunti ya Saint Louis wana siku tatu pekee za kuwasilisha maombi kwa ajili ya msaada wa majanga wa Fema. Wamiliki nyumba na wapangaji wa Missouri ambao walikuwa na uharibifu wa mali au hasara iliyosababishwa na dhoruba na mafuriko au wale majengo yao ya kupanga yaliharibiwa na wakalazimika kuhama, huenda wakastahili kupokea msaada wa serikali wa majanga.

Kuna njia kadhaa za wapangaji na wamiliki wa nyumba ambao waliathiriwa na majanga ya Julai kuomba msaada wa majanga ya FEMA.

  • Ikiwa unatumia huduma ya kupitisha ujumbe, kama vile kupitisha ujumbe kupitia video (VRS), simu iliyo na maelezo mafupi au huduma nyingine, pea FEMA nambari ya huduma hiyo. Nambari ya Msaada inafunguliwa siku saba kwa wiki. Bonyeza 2 kwa Kihispania au 3 ili kupata mkalimani anayezungumza lugha yako.
  • Wanusurikaji wanaweza kuomba msaada ana kwa ana katika kituo cha msaada wa majanga (DRC)

Chuo cha Ranken Technical

Kituo cha Mary Ann Lee Technology

1313 N. Newstead Ave.

St. Louis, MO 63113

(Kona ya Newstead na Page)

  • Kinafunguliwa Jumatatu-Ijumaa, saa mbili asubuhi (8am) hadi saa kumi na mbili jioni (6 p.m.) na Jumamosi, saa mbili asubuhi (8am) hadi saa kumi na moji jioni (5 p.m.)

Hakuna miadi inahitajika kutembelea Kituo cha Msaada wa Majanga (DRC). Wanaokuja bila miadi wanakaribishwa.

Unapotuma ombi kwa FEMA, uwe na maelezo yafuatayo tayari:

• Nambari ya simu ambayo unaweza kupigiwa

• Anwani wakati wa mafuriko

• Anwani unapoishi sasa

• Nambari ya Ruzuku ya Serikali ya Mtu mmoja katika familia

• Orodha ya msingi ya uharibifu na hasara

• Taarifa za benki ukichagua kuwekewa moja kwa moja pesa za FEMA kwenye benki

• Taarifa za Bima ikiwa una bima, ikijumuisha nambari ya sera

Ikiwa una bima ya wamiliki nyumba, mpangaji au mafuriko, unapaswa kuwasilisha dai haraka iwezekanavyo. FEMA haiwezi kulipia tena hasara zinazolipiwa na bima. Ikiwa sera yako haishughulikii gharama zako zote za uharibifu, unaweza kustahili usaidizi wa serikali.

Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA na @FEMARegion7.

Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov na FEMA.gov/disaster/4665.

Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho