Msaada wa FEMA Hautaathiri Udhamini Mwingine

Release Date:
Agosti 1, 2023

Kujiandikisha ili kupata msaada wa majanga kutoka kwa FEMA hakutaathiri ustahilifu wako wa udhamini mwingine wa serikali.

Ruzuku za FEMA si mapato yanayotozwa kodi, na unaweza kuzipokea bila kupunguza au kuondoa udhamini wowote wa serikali au jimbo unayostahili kwa sasa. Hii inajumuisha udhamini wa ruzuku ya serikali, Medicare na Medicaid, pamoja na yale unayopokea kupitia jimbo la Vermont, ikijumuisha Mpango wa Msaada wa Lishe ya Ziada (SNAP) na Reach Up, au Msaada wa Muda kwa Familia Zilizo na uhitaji.

Iwapo uliathiriwa na mafuriko katika kaunti za Caledonia, Chittenden, Lamoille, Orange, Orleans, Rutland, Washington, Windham na Windsor, FEMA inaweza kukusaidia kulipia gharama zilizosababishwa na majanga zisizogharamiwa na bima au vyanzo vingine. Ili kupata maelezo zaidi au kutuma ombi, tembelea DisasterAssistance.gov, pakua FEMA App au piga Simu ya Usaidizi ya FEMA kwa 800-621-3362. Tafsiri ya lugha inapatikana; ikiwa unatumia huduma ya usambazaji kama vile huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo unapotuma ombi.

Kwa taarifa mpya zaidi kuhusu itikio na kurejelea hali ya kawaida Vermont, tembelea fema.gov/disaster/4720. Fuata akaunti ya FEMA Region 1 kwenye Twitter katika twitter.com/FEMARegion1 au FEMA Facebook katika facebook.com/FEMA.. Fuata Wakala wa Usimamizi wa Dharura wa Vermont katika  twitter.com/vemvt kwenye Twitter na kwenye Facebook katika  facebook.com/VermontEmergencyManagement

FEMA imejitolea kuhakikisha msaada wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza, au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa maafa au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi kuwa ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wanaotumia lugha nyingi wanapatikana.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho