Kuelewa Barua Yako ya FEMA

Release Date Release Number
003
Release Date:
Julai 19, 2023

BURLINGTON, VT – Wakazi wa Vermont  walioomba msaada kutoka FEMA kutokana na mafuriko na dhoruba kali, mnamo tarehe 7 Julai, 2023 na kuendelea, watapokea barua rasmi ya uamuzi kutoka FEMA. Inaweza kubainisha kuwa hustahili msaada, lakini haina manaa kuwa umekataliwa.

Ni muhimu kusoma barua kwa makini kwa sababu imejumuisha kiasi cha msaada ambao FEMA itatoa na maelezo kuhusu matumizi sahihi ya fedha za msaada wa maafa. Barua hii pia itafafanua hali ya ombi lako na kukushauri hatua unazotakiwa kufuata ili kukata rufaa dhidi ya uamuzi usiokupendeza.

Mara kwa mara, utahitaji tu kutuma maelezo zaidi  au hati za uthibitisho kwa FEMA ili uendelee kukagua ombi lako la msaada wa kifedha. Mifano ya hati zinazokosekana inaweza kujumuisha:

  • Uthibitisho wa bima ya maafa
  • Makubaliano ya madai ya bima au barua ya kukataliwa kutoka kwa mtoa huduma wa bima
  • Uthibitisho wa utambulisho
  • Uthibitisho wa makazi 
  • Uthibitisho wa umiliki
  • Uthibitisho kwamba mali iliyoharibika ilikuwa makazi ya msingi ya mwombaji wakati maafa yanatokea.

Iwapo una maswali kuhusu barua yako, piga Simu ya Dharura ya Usaidizi wa Maafa kwenda nambari 800-621-3362. Wataalamu wanapatikana siku saba kwa wiki, siku 365 kwa mwaka, huduma za kutafsiri lugha zinapatikana. Ikiwa unatumia huduma ya kuwasiliana moja kwa moja kama vile Huduma ya Kuwasiliana Moja kwa Moja ( Video Relay Service), huduma ya simu ya manukuu au nyinginezo, toa nambari ya huduma hiyo kwa FEMA unapotuma ombi.

Kukata Rufaa Dhidi ya Uamuzi wa FEMA

Iwapo hukubaliani na uamuzi wa FEMA au kiasi cha msaada kulichotolewa, unaweza kutuma barua ya kukata rufaa na hati za kuthibitisha dai lako, kama vile makadirio ya mkandarasi kwa ajili ya ukarabati wa nyumba. Una siku 60 kutoka tarehe ya barua yako ya uamuzi ya FEMA ili kukata rufaa yako kwa FEMA.

Kwa mujibu wa sheria, FEMA haiwezi kukupa ruzuku wakati vyanzo vingine, kama vile bima, ufadhili wa watu wengi au msaada wa kifedha kutoka kwa mashirika yasiyo ya faida yamelipa gharama ya mahitaji sawa yanayohusiana na maafa. Kwa maneno mengine, FEMA haiwezi kulipia gharama za ukarabati wa nyumba ikiwa tayari umepokea pesa kutoka kwa kampuni yako ya bima kwa ajili ya ukaratiba huo.

Hata hivyo, wale waliolipwa kiasi kidogo kulingana na bima zao wanaweza kupokea msaada kwa mahitaji ambayo hayajafikiwa baada ya madai ya bima kushughulikiwa. Ingawa FEMA inaweza kutoa msaada wa mahitaji ya msingi, haitoi msaada wa kugharamia fidia za bima.

Rufaa zinapaswa kuwa kwenye mfumo wa maandishi katika barua iliyotiwa saini na tarehe, ikielezea sababu za kukata rufaa. Inapaswa pia kujumuisha: 

  • Jina kamili la mwombaji 
  • Nambari ya maafa(DR-4720 -VT)
  • Anwani ya makazi ya msingi kabla ya maafa 
  • Anwani na nambari ya simu ya sasa ya mwombaji 
  • Nambari yako ya maombi ya FEMA yenye tarakimu tisa kwenye hati zote

Iwapo mtu mwingine tofauti na mwombaji au mwombaji mwenza ameandika barua ya rufaa, mtu huyo lazima atie saini na kuwasilisha kwa FEMA taarifa iliyotiwa saini inayoidhinisha mtu huyo kushughulikia suala hilo kwa niaba ya mwombaji. 

Rufaa lazima ziwekewe stempu ya posta ndani ya siku 60 kutoka tarehe iliyobainishwa kwenye barua yako ya uamuzi ya FEMA. Barua za rufaa na hati za uthibitisho zinaweza kupakiwa kwenye akaunti yako binafsi ya mtandaoni ya FEMA. Ili kuweka mipangilio kwenye akaunti, tembelea DisasterAssistance.gov kisha ufuate maelekezo. 

Mbinu nyingine za kuwasilisha hati zinajumuisha:

Barua pepe: FEMA National Processing Service Center, S.L.P 10055, Hyattsville MD 20782-7055

Fax: 800-827-8112 Attention: FEMA 

Ili utazame video ya Lugha ya Ishara ya Marekani (American Sign Language) video kuhusu jinsi ya kutuma maombi, nenda kwenye: www.youtube.com/watch?v=M1a6lYO5hgY 

Kwa taarifa za hivi punde kuhusu kukabiliana na maafa ya dhoruba kali na mafuriko katika eneo la Vermont, tembelea  FEMA.gov/Disaster/4720. Unaweza pia kufuatilia facebook.com/FEMA.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho