Kuelewa Barua yako ya FEMA

Release Date:
Agosti 8, 2023

Manusura wa majanga katika kaunti za Caledonia, Chittenden, Lamoille, Orange, Orleans, Rutland, Washington, Windham na Windsor waliotuma maombi ya msaada kutoka kwa FEMA kwa ajili ya dhoruba kali za Julai, mafuriko, maporomoko ya ardhi na matope watapokea barua ya uamuzi wa ustahilifu kutoka kwa FEMA kupitia barua au barua pepe.

Huenda ikasema kwamba hustahili msaada, lakini hiyo sio kukataliwa.

Ni muhimu kusoma barua kwa makini kwa sababu itajumuisha kiasi cha msaada ambacho FEMA inaweza kutoa na taarifa kuhusu matumizi sahihi ya fedha za msaada wa majanga. Barua hiyo pia itaeleza hali ya ombi lako na kukushauri kuhusu unachohitaji kufanya ili kukata rufaa dhidi ya uamuzi usiokupendeza.

Mara nyingi, unahitaji tu kutuma maelezo zaidi au hati za kutegemeza ombi lako kwa FEMA ili kuendelea kukagua ombi lako la msaada wa kifedha. Mifano ya hati zinazokosekana zinaweza kujumuisha:

 • Uthibitisho wa malipo ya bima;
 • Ulipaji wa madai ya bima au barua ya kunyimwa kutoka kwa mhudumu wa bima;
 • Uthibitisho wa utambulisho;
 • Uthibitisho wa ukaaji;
 • Uthibitisho wa umiliki; au
 • Uthibitisho kwamba mali iliyoharibiwa ilikuwa makazi ya msingi ya mwombaji wakati wa majanga.

Ikiwa una maswali kuhusu barua yako, piga simu ya kwa laini ya msaada wa majanga 800-621-3362. Wataalamu wanapatikana siku saba kwa wiki, siku 365 kwa mwaka, na huduma za kutafsiri lugha zinapatikana. Ukitumia huduma ya mawasiliano kama vile Video Relay Service (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo unapotuma ombi.

Au unaweza kutembelea Kituo cha Msaada wa Majanga kupata msaada wa ana kwa ana, ambapo wataalamu wa FEMA wanaweza kusaidia na maombi, kujibu maswali na kutoa marejeleo ya rasilimali. Ili kupata kituo karibu nawe, tembelea fema.gov/drc .

Kukata rufaa dhidi ya Uamuzi wa FEMA

Ikiwa hukubaliani na uamuzi wa FEMA au kiasi cha msaada uliotolewa, unaweza kuwasilisha barua ya rufaa na hati zinazounga mkono dai lako, kama vile makadirio ya mkandarasi kwa ajili ya ukarabati wa nyumba. Una siku 60 kutoka tarehe ya barua yako ya uamuzi ya FEMA ili kutuma rufaa yako kwa FEMA. 

Kwa mujibu wa sheria, FEMA haiwezi kukupa msaada wakati chanzo kingine chochote - bima, ufadhili wa watu wengi au msaada wa kifedha kutoka kwa mashirika ya kujitolea - kimelipia gharama ya mahitaji sawa yanayohusiana na majanga. Kwa maneno mengine, FEMA haiwezi kulipia marekebisho ya nyumba ikiwa tayari umepokea pesa kutoka kwa kampuni yako ya bima kwa ajili ya marekebisho sawa.

Hata hivyo, wale ambao hawana bima ya kutosha wanaweza kupata msaada kwa mahitaji ambayo hayajashughulikiwa baada ya madai ya bima kutatuliwa. Ingawa FEMA inaweza kutoa msaada wa mahitaji ya msingi, haitoi msaada wa kugharamia makato ya bima.

Katika barua iliyotiwa sahihi na tarehe, eleza sababu ya kukata rufaa. Rufaa lazima ziwe katika maandishi, na zijumuishe:

 • Jina kamili la mwombaji
 • Nambari ya Janga (DR-4720 -VT)
 • Anwani ya makazi ya msingi kabla ya janga
 • Nambari ya simu ya sasa na anwani ya mwombaji
 • Nambari yako ya maombi ya FEMA yenye tarakimu tisa kwenye hati zote

Iwapo mtu mwingine mbali na mwombaji au mwombaji mwenza ataandika barua ya rufaa, mtu huyo lazima atie sahihi na kuandalia FEMA taarifa iliyotiwa sahihi inayoidhinisha mtu huyo kutenda kwa niaba ya mwombaji.

Rufaa lazima ziwekewe alama ya posta ndani ya siku 60 tangu tarehe iliyo kwenye barua yako ya uamuzi ya FEMA. Barua za rufaa na hati zinazounga mkono zinaweza kupakiwa kwenye akaunti yako ya kibinafsi ya mtandaoni ya FEMA. Ili kufungua akaunti, tembelea DisasterAssistance.gov na ufuate maelekezo.

Njia zingine za kuwasilisha hati ni pamoja na:

 • Barua: FEMA National Processing Service Center, P.O. Box 10055, Hyattsville MD 20782-7055
 • Faksi: 800-827-8112 Attention: FEMA 

Kupata taarifa mpya zaidi kuhusu shughuli za msaada Vermont, tembelea fema.gov/disaster/4720. Fuata akaunti ya FEMA Region 1 kwenye Twitter katika twitter.com/FEMARegion1 au FEMA Facebook katika facebook.com/FEMA. Fuata Wakala wa Usimamizi wa Dharura wa Vermont katika twitter.com/vemvt kwenye Twitter na kwenye Facebook katika facebook.com/VermontEmergencyManagement.

FEMA imejitolea kuhakikisha msaada wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza, au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa majanga au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi kuwa ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Waendeshaji wa lugha nyingi wanapatikana.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho