Kwa uratibu wa jimbo na washirika wa ndani, tutafunga kabisa Kituo cha Kushughulikia Maafa (DRC) cha Island Pond saa 6 p.m. Jumamosi, tarehe 12 Oktoba, 2024.
Kituo hiki kwa sasa hufunguliwa saa 9 a.m. hadi saa 6 p.m. Jumatatu hadi Jumamosi:
- Brighton Town Hall Gym, 49 Mill Street, Island Pond, VT 05846
Kufungwa kwa vituo hivi vya muda kunaratibiwa na jimbo na washirika wa ndani kwa ujumla, kulingana na idadi ya watembeaji na mahitaji ya jamii.
Kituo kipya cha DRC mjini Newport kimepangwa kufunguliwa Jumatano, tarehe 16 Oktoba 2024. Kuanzia Oktoba 16, kituo hiki kipya kitakuwa wazi kuanzia saa 9:00 a.m. hadi saa 6:00 p.m., Jumatatu hadi Jumamosi, katika:
- Newport City Municipal Building - 222 Main Street, Newport, VT 05855
Kufungwa kwa Likizo za Serikali Kuu
Vituo vya Kushughulikia Majanga vya Vermont vitafungwa Jumatatu, tarehe 14 Oktoba ili kuadhimisha Siku ya Wazawa na Siku ya Columbus. Vitafunguliwa tena Jumanne, tarehe 15 Oktoba saa za kawaida.
Wakazi wa Vermont walioathiriwa na dhoruba zote mbili za Julai wanaweza kutembelea Kituo cha Kushughlikia Majanga ili kupata msaada wa ana kwa ana kutoka FEMA na Utawala wa Biashara Ndogo wa Marekani. Kwa taarifa za hivi punde kuhusu sehemu na saa, tembelea fema.gov/drc.
Pia kuna njia zingine tatu za kuomba ambazo hazihitaji kutembelea kituo:
- Nenda mtandaoni kwa DisasterAssistance.gov.
- Piga Simu ya Usaidizi ya FEMA kwa 800-621-3362.
- Pakua Programu ya Simu ya FEMA.