Wiki Moja Imesalia kwa Wakazi wa Missouri Kuomba Usaidizi wa Kibinafsi wa FEMA

Release Date Release Number
24
Release Date:
Oktoba 31, 2022

Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles zimebakia na wiki moja pekee kutuma maombi ya msaada wa majanga ya FEMA kabla ya tarehe ya mwisho ya Novemba 7. Wamiliki wa nyumba na wapangaji wa Missouri ambao walikuwa na uharibifu wa mali au hasara iliyosababishwa na dhoruba kali na mafuriko ya Julai 25-28, au wale ambao nyumba zao ziliharibiwa na kulazimika kuhama, huenda wakastahili kupokea msaada wa serikali wa majanga.

Kuna njia kadhaa za wapangaji na wamiliki wa nyumba ambao waliathiriwa na majanga ya Julai kuomba msaada wa majanga ya FEMA.

  • Ikiwa unatumia huduma ya kupitisha ujumbe, kama vile kupitisha ujumbe kupitia video (VRS), simu iliyo na maelezo mafupi au huduma nyingine, pea FEMA nambari ya huduma hiyo. Nambari ya Msaada inafunguliwa siku saba kwa wiki. Bonyeza 2 kwa Kihispania au 3 ili kupata mkalimani anayezungumza lugha yako.
  • Walionusurika wanaweza pia kutuma maombi ana kwa ana katika Vituo viwili vya Msaada wa Majanga (DRC).

University City Recreation Division

Centennial Commons

7210 Olive Blvd.

University City, MO 63130

Itafungwa kabisa Jumatano, Novemba 2 saa kumi na moja jioni (5 p.m)         

Chuo cha Ranken Technical

Kituo cha Mary Ann Lee Technology

1313 N. Newstead Ave.

St. Louis, MO 63113

(Kona ya Newstead na Page)

  • Inafunguliwa Jumatatu-Ijumaa, saa mbili asubuhi (8am) hadi saa kumi na mbili jioni (6 p.m.) na Jumamosi, saa mbili asubuhi (8am) hadi saa kumi na moji jioni (5 p.m.)

Hakuna miadi inahitajika kutembelea Kituo cha Msaada wa Majanga (DRC). Wanaokuja bila miadi wanakaribishwa.

Unapotuma ombi kwa FEMA, uwe na maelezo yafuatayo tayari:

• Nambari ya simu ambayo unaweza kupigiwa

• Anwani wakati wa mafuriko

• Anwani unapoishi sasa

• Nambari ya Ruzuku ya Serikali ya Mtu mmoja katika familia

• Orodha ya msingi ya uharibifu na hasara

• Taarifa za benki ukichagua kuwekewa moja kwa moja pesa za FEMA kwenye benki

• Taarifa za Bima ikiwa una bima, ikijumuisha nambari ya sera

Ikiwa una bima ya wamiliki nyumba, mpangaji au mafuriko, unapaswa kuwasilisha dai haraka iwezekanavyo. FEMA haiwezi kulipia tena hasara zinazolipiwa na bima. Ikiwa sera yako haishughulikii gharama zako zote za uharibifu, unaweza kustahili usaidizi wa serikali.

Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA na @FEMARegion7.

Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov na FEMA.gov/disaster/4665.

Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho