Zaidi ya dola milioni 54 za ufadhili wa serikali zimeidhinishwa kwa ajili ya watu walioathiriwa na mafuriko ya Julai 25-28 na dhoruba kali katika eneo la St. Louis huko Missouri.
- FEMA imeidhinisha dola milioni 28.7 katika ruzuku ya Usaidizi wa Mtu Binafsi kwa wapangaji na wamiliki wa nyumba kwa ajili ya uharibifu na mahitaji makubwa ambayo hayalipwi na bima.
- Mpango wa Kitaifa wa Bima ya Mafuriko ya FEMA umelipa madai ya dola milioni 14.4 kwa wamiliki wa bima ya mafuriko.
- Utawala wa Biashara Ndogo za Marekani umeidhinisha dola milioni 11.2 katika mikopo ya majanga kwa ajili ya wamiliki wa nyumba, wapangaji na biashara.
Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi na FEMA ni tarehe 7 Oktoba.
Watu walioathiriwa na majanga katika Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles wana njia tatu za kutuma maombi na kuwasiliana na FEMA:
Piga simu: 1-800-621-FEMA (3362)
- Enda kwenye mtandao: DisasterAssistance.gov
- Tembelea kituo cha Msaada wa Majanga
Ikiwa unatumia huduma ya relay, kama vile video relay (VRS), simu iliyo na maelezo mafupi au huduma nyingine, pea FEMA nambari ya huduma hiyo. Opereta wa nambari ya usaidizi wanapatikana kutoka kumi na mbili asubuhi (6am) hadi nne usiku (10pm) kila siku. Bonyeza 2 kwa Kihispania. Bonyeza 3 ili kupata mkalimani anayezungumza lugha yako.
Vituo Sita vya Msaada wa Majanga viko Wazi kutoa Msaada wa Moja kwa Moja
Wataalamu wa Misaada kutoka FEMA na Usimamizi wa Biashara Ndogo Marekani wanasaidia watu kukamilisha au kuangalia hali ya maombi yao katika maeneo haya:
JIJI LA ST. LOUIS
Chuo cha Ranken Technical
Kituo cha Teknolojia cha Mary Ann Lee
1313 N. Newstead Ave.
St. Louis, MO 63113
(Kwenye kona ya Newstead na Page)
KAUNTI YA ST. LOUIS
Kituo cha Urban League Empowerment
9420 W. Florissant Ave.
Ferguson, MO 63136
KAUNTI YA ST. LOUIS
Kituo cha University City Recreation
Centennial Commons
7210 Olive Blvd.
University City, MO 63130
Kituo cha Hazelwood Civic
8969 Dunn Road
Hazelwood, MO 63042
KAUNTI YA ST. CHARLES
Kituo cha Manispaa ya O'Fallon
100 N. Main St.
O’Fallon, MO 63366
(Kiingilio cha Kusini-mashariki)
Bodi ya Rasilimali za Ulemavu Unaoendelea – Jengo la DDRB
1025 Country Club Road
St. Charles, MO 63303
(I-70 karibu na njia ya kutoka Zumbehl)
- Masaa katika maeneo yote: saa Mbili asubuhi (8 a.m.)–saa Moja jioni (7 p.m.). Jumatatu-Jumamosi hadi notisi nyingine itolewe
- Hakuna miadi inahitajika kutembelea Kituo cha Msaada wa Majanga. Wanaokuja bila miadi wanakaribishwa.
- Ikiwa unahitaji msaada kutuma maombi, FEMA inaweza kukusaidia katika Kituo cha Msaada wa Majanga.
Kuhusu Usaidizi wa Mtu Binafsi wa FEMA
Kwa mahitaji ambayo hayajashughulikiwa na bima au vyanzo vingine, FEMA inaweza kutoa pesa za ruzuku ya Usaidizi wa Mtu Binafsi ambazo si lazima zilipwe kwa:
- Msaada wa Kodi ya Nyumba ikiwa unahitaji kuhama kwa sababu ya uharibifu wa mafuriko
- Mali ya kibinafsi ambayo iliharibika au kuharibiwa na mafuriko
- Kurudishiwa Malipo ya Mahali pa kulala ikiwa ulilazimika kukaa katika hoteli kwa muda
- Marekebisho ya Msingi ya Nyumba kwa wamiliki wa nyumba ambao makazi yao ya msingi yaliharibiwa na mafuriko
- Mahitaji Mengine Muhimu yaliyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni
Mbali na msaada ulioorodheshwa, tafadhali kumbuka yafuatayo:
- Ombi moja tu kwa kila familia
- FEMA hailipii chakula kilichopotea au kuharibika
- FEMA hufanya kazi na kila mtu - wapangaji na wamiliki wa nyumba - kwa msingi wa kesi baada ya kesi.
- Kisheria, Fema hairuhusiwi kulipia tena malipo ya bima au usaidizi uliotolewa na vyanzo vingine.
Wamiliki wa Nyumba na Wapangaji: Ikiwa umetumwa kwa SBA kwa ajili ya mkopo wa majanga, tafadhali wasilisha ombi. Kuwasilisha ombi la SBA hukuwezesha kuzingatiwa kwa ajili ya ruzuku za ziada. Ikiwa unastahili kupata mkopo, utakuwa na rasilimali hiyo ikiwa utachagua kuukubali.
Usaidizi mwingine unapatikana kwa kupiga simu kwa 2-1-1 United Way 211 huunganisha watu binafsi wenye mahitaji ambayo hayajatimizwa kwa programu za usaidizi kupitia mashirika ya kujitolea na ya kidini. Yeyote aliyeathiriwa anayehitaji usaidizi wa ziada anapaswa kupiga simu kwa 2-1-1 kwa usaidizi au atembelee http://211helps.org.
Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA na @FEMARegion7.
Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov na FEMA.gov/disaster/4665.
Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi.