FEMA inatoa maelezo bila malipo kuhusu jinsi ya kufanya nyumba yako iwe imara na salama - iwe iliharibiwa na mafuriko msimu huu wa kiangazi au la.
Unaweza kuzungumza moja kwa moja na wataalamu wa FEMA katika maduka ya kuboresha nyumba yaliyo karibu.
Wanaojifanyia marekebisho wenyewe na wataalamu wanaweza kupata majibu ya maswali na kujadili:
- Mbinu zilizothibitishwa za kuzuia uharibifu kutokana na majanga wakati ujao
- Mbinu za kujenga upya nyumba
- Vidokezo vya kupunguza hatari yako ya majanga - iwe unamiliki au unakodisha nyumba yako
Eneo:
The Home Depot
11215 St Charles Rock Rd
Bridgeton, MO 63044
The Home Depot
1603 S Hanley Rd
Brentwood, MO 63144
The Home Depot
3202 S Kingshighway Blvd
Saint Louis, MO 63139
Tarehe na Masaa:
Jumatatu, Oktoba 17, hadi Jumamosi, Oktoba 22, saa mbili asubuhi (8 a.m.)—saa kumi na mbili jioni (6 p.m.)
Jumatatu, Oktoba 24, hadi –Jumatano, Oktoba 26, saa mbili asubuhi (8 a.m.)—saa kumi na mbili jioni (6 p.m.)
Alhamisi, Oktoba 27, saa mbili asubuhi (8 a.m.).–saa nane alasiri (2 p.m.)
Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA na @FEMARegion7.
Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov na FEMA.gov/disaster/4665.
Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi.