Kituo cha msaada wa majanga cha FEMA kitafunguliwa katika Ferguson (Kaunti ya St. Louis) mnamo Jumanne, Agosti 30 ili kutoa usaidizi wa moja kwa moja kwa watu walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko na dhoruba kali Julai 25—28.
Wataalamu wa Misaada kutoka FEMA na Usimamizi wa Biashara Ndogo Marekani watatoa taarifa kuhusu huduma zinazopatikana, kueleza mipango ya usaidizi na kuwasaidia walionusurika kukamilisha au kuangalia hali ya maombi yao.
Kituo cha msaada wa majanga kinapatikana katika:
Kituo cha Urban League Empowerment
9420 W Florissant Ave.
Ferguson, MO 63136
SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.) siku saba kwa wiki hadi notisi nyingine itolewe
Vituo vingine vya msaada vimefunguliwa katika:
KAUNTI YA ST. LOUIS
Kituo cha University City Recreation
Centennial Commons
7210 Olive Blvd
University City, MO 63130
SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.) siku saba kwa wiki hadi notisi nyingine itolewe
Kituo cha Hazelwood Civic
8969 Dunn Road
Hazelwood, MO 63042
SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.) siku saba kwa wiki hadi notisi nyingine itolewe
JIJI LA ST. LOUIS
Chuo cha Ranken Technical
Kituo cha Teknolojia cha Mary Ann Lee
1313 N. Newstead Ave.
St. Louis, MO 63113
(Kwenye kona ya Newstead na Page)
SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.) siku saba kwa wiki hadi notisi nyingine itolewe
KAUNTI ST. CHARLES
Bodi ya Rasilimali za Ulemavu Unaoendelea – Jengo la DDRB
1025 Country Club Road
St. Charles, MO 63303
(I-70 karibu na njia ya kutoka Zumbehl)
SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.) siku saba kwa wiki hadi notisi nyingine itolewe
Hakuna miadi inahitajika kutembelea Kituo cha Msaada wa Majanga. Wanaokuja bila miadi wanakaribishwa.
Vituo vyote vya Msaada wa Majanga vitafunguliwa Siku ya Wafanyakazi (Labor Day), Jumatatu, Septemba 5
Kabla ya kutembelea kituo, tuma ombi na FEMA mtandaoni kwenye DisasterAssistance.gov au piga simu 800-621-FEMA (3362).
Watu walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko katika Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles wanaweza kutembelea kituo chochote cha msaada.
Kwa mahitaji yanayohusiana moja kwa moja na mafuriko ya Julai 25—28, FEMA inaweza kutoa pesa za ruzuku ya Usaidizi wa Mtu Binafsi ambazo si lazima zilipwe kwa:
- Msaada wa Kodi ya Nyumba ikiwa unahitaji kuhama kwa sababu ya uharibifu wa mafuriko
- Mali ya kibinafsi ambayo iliharibika au kuharibiwa na mafuriko
- Kurudishiwa Malipo ya Mahali pa kulala ikiwa ulilazimika kukaa katika hoteli kwa muda
- Marekebisho ya Msingi ya Nyumba kwa wamiliki wa nyumba ambao makazi yao ya msingi yaliharibiwa na mafuriko
- Mahitaji Mengine Muhimu yaliyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni
Mbali na msaada ulioorodheshwa, tafadhali kumbuka yafuatayo:
- Ombi moja tu kwa kila familia
- FEMA hailipii chakula kilichopotea au kuharibika
Kisheria. Fema hairuhusiwi kulipia tena malipo ya bima au usaidizi uliotolewa na vyanzo vingine.
Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA na @FEMARegion7.
Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov na FEMA.gov/disaster/4665.
Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi.