KITUO CHA MSAADA WA MAJANGA KATIKA UNIVERSITY CITY, MISSOURI KITAFUNGWA WIKI IJAYO [https://www.fema.gov/sw/press-release/20221026/disaster-recovery-center-university-city-missouri-close-next-week] Release Date: Oktoba 26, 2022 Kituo cha Msaada wa Majanga katika University City kitafungwa kabisa Jumatano, Novemba 2 saa kumi na moja jioni (5pm) CENTENNIAL COMMONS (RECREATION CENTER) 7210 OLIVE BLVD. UNIVERSITY CITY, MO 63130 Kituo kimoja cha Msaada wa Majanga kitabakia wazi ili kuwasaidia waathiriwa walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko ya Julai 25-28 na dhoruba kali: Chuo cha Ranken Technical Kituo cha Mary Ann Lee Technology 1313 N. Newstead Ave. St. Louis, MO 63113 (Karibu na Kona ya Newstead na Page) ISIPOKUWA IBAINISHWE VINGINEVYO, MASAA ZA KITUO CHA MSAADA NI: Jumatatu – Ijumaa, saa mbili asubuhi (8 a.m.)– saa kumi na mbili jioni (6 p.m.) Jumamosi, saa mbili asubuhi (8 a.m.) – saa kumi na moja jioni (5 p.m.) Inafungwa Jumapili Katika vituo vya msaada, wataalamu kutoka FEMA na Usimamizi wa Biashara Ndogo ya Marekani wanatoa maelezo kuhusu huduma zinazopatikana, wakifafanua programu za usaidizi na kuwasaidia walionusurika kukamilisha au kuangalia hali ya maombi yao. * TUMA OMBI KWA FEMA MTANDAONI KUPITIA DISASTERASSISTANCE.GOV [https://www.disasterassistance.gov/] AU PIGA SIMU KWA 800-621-FEMA (3362). * IWAPO UNAHITAJI USAIDIZI KUTUMA OMBI, FEMA INAWEZA KUKUSAIDIA KATIKA KITUO CHA MSAADA WA MAJANGA. * HAKUNA MIADI INAHITAJIKA KUTEMBELEA KITUO CHA MSAADA WA MAJANGA. WANAOKUJA BILA MIADI WANAKARIBISHWA. * WATU WALIOATHIRIWA MOJA KWA MOJA NA MAFURIKO KATIKA JIJI LA ST. LOUIS, KAUNTI YA ST. LOUIS NA KAUNTI YA ST. CHARLES WANAWEZA KUTEMBELEA KITUO CHOCHOTE CHA MSAADA KUPATA USAIDIZI WA ANA KWA ANA. KIKUMBUSHA: TAREHE YA MWISHO YA KUTUMA MAOMBI YA FEMA NI NOVEMBA 7.                                                  Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA [https://twitter.com/mosema_] na @FEMARegion7 [https://twitter.com/femaregion7]. Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov [https://recovery.mo.gov/] na FEMA.gov/disaster/4665 [https://www.fema.gov/disaster/4665]. _Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi._