FEMA INATOA USHAURI WA KUREKEBISHA NA KUJENGA UPYA BILA MALIPO KATIKA MADUKA YALIYO KARIBU [https://www.fema.gov/sw/press-release/20220929/fema-offers-free-repair-and-rebuilding-advice-local-stores] Release Date: Septemba 29, 2022 FEMA inatoa maelezo bila malipo kuhusu jinsi ya kufanya nyumba yako iwe imara na salama zaidi - iwe iliharibiwa na mafuriko msimu huu wa kiangazi au la. Kuwekeza sasa kunaweza kusaidia kuzuia au kupunguza uharibifu mkubwa wa mafuriko siku zijazo. Unaweza kuzungumza moja kwa moja na wataalamu wa FEMA katika maduka ya kuboresha nyumba yaliyo karibu. Wanaojifanyia marekebisho wenyewe na wataalamu wanaweza kupata majibu ya maswali na kujadili: * Mbinu zilizothibitishwa za kuzuia uharibifu kutokana na majanga wakati ujao * Mbinu za kujenga upya nyumba * Vidokezo vya kupunguza hatari yako ya majanga - iwe unamiliki au unakodisha nyumba yako ENEO: THE HOME DEPOT 10930 NEW HALLS FERRY RD SAINT LOUIS, MO 63136 THE HOME DEPOT 3891 MEXICO RD SAINT CHARLES, MO 63303 THE HOME DEPOT 1525 STATE HWY K O’FALLON, MO 63366 THE HOME DEPOT 8901 PAGE AVENUE OVERLAND, MO 63114                                                    TAREHE: Jumatatu, Oktoba 3, hadi Jumamosi, Oktoba 15 MASAA: Jumatatu—Jumamosi, saa tatu asubuhi (9 a.m.)—saa moja jioni (7 p.m.) na Jumapili saa nne asubuhi (10 a.m.)—saa tisa alasiri (3 p.m.) Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA [https://twitter.com/mosema_] na @FEMARegion7 [https://twitter.com/femaregion7]. Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov [https://recovery.mo.gov/] na FEMA.gov/disaster/4665 [https://www.fema.gov/disaster/4665]. _Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi._