WAKAZI WA KAUNTI YA DUTCHESS WALIOATHIRIWA NA KIMBUNGA IDA SASA WANAWEZA KUTUMA MAOMBI YA USAIDIZI WA FEMA [https://www.fema.gov/sw/press-release/20211026/dutchess-county-residents-affected-hurricane-ida-can-now-apply-fema] Release Date: Oktoba 25, 2021 NEW YORK –FEMA imeongeza Kaunti ya Dutchess kwenye tangazo la serikali la janga la Septemba 5 kwa sababu ya Kimbunga Ida, na hivyo kufanya idadi ya kaunti ambazo wakazi wake sasa wanastahili kutuma maombi ya usaidizi ya janga ya FEMA kufika tisa. Wakazi wa kaunti za BRONX, DUTCHESS, KINGS, NASSAU, QUEENS, RICHMOND, ROCKLAND, SUFFOLK NA WESTCHESTER sasa wanaweza kutuma maombi ya programu ya Usaidizi ya Mtu Binafsi ya FEMA. Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni JUMATATU, DESEMBA 6. Wale ambao tayari wametuma maombi hawahitaji kutuma maombi tena. Kimbunga Ida kilipiga New York Septemba 1-3. Wamiliki wa nyumba na wapangaji katika kaunti tisa ambao walipata uharibifu au hasara kutokana na dhoruba hiyo wanahimizwa kutuma maombi ya usaidizi. Usaidizi wa janga unaweza kujumuisha msaada wa kusaidia kulipia makazi ya muda na marekebisho muhimu ya nyumba pamoja na mahitaji mengine makubwa yanayohusiana na janga kama vile gharama za matibabu na meno. Unapaswa kutuma maombi kwa FEMA hata kama una bima, lakini kwanza tuma dai kwa mtoa huduma wako wa bima. FEMA hutoa usaidizi kwa waombaji kwa gharama zao zisizo na bima au zisizo na bima ya kutosha iliyosababishwa na janga na mahitaji makubwa. Waombaji wanahitajika kujulisha FEMA kuhusu bima yote ikijumuisha mafuriko, wamiliki wa nyumba na gari. Ni lazima waombaji walio na bima watoe hati zinazobainisha malipo au manufaa yao ya bima kabla ya FEMA kuzingatia ustahilifu wao kwa aina za usaidizi ambazo zinaweza kulipwa na bima ya kibinafsi. Ili kutuma ombi la usaidizi wa FEMA, tembelea DisasterAssistance.gov [http://www.disasterassistance.gov/], tumia programu ya simu ya FEMA au piga simu kwa NAMBARI YA USAIDIZI YA FEMA kwa 800-621-3362. Ikiwa unatumia huduma ya uwasilishaji wa video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyingine, pea FEMA nambari ya huduma hiyo. Waendeshaji wa nambari ya usaidizi wanapatikana kutoka 2 asubuhi hadi 1 jioni. kila siku. Bonyeza 2 kwa Kihispania. Bonyeza 3 ili kupata mkalimani anayezungumza lugha yako. Unaweza pia kutembelea Kituo cha Kushughulikia Majanga na kukutana ana kwa ana na wafanyakazi wa FEMA na wawakilishi wa mashirika mengine ya serikali na mawakala wa jimbo ambao wanaweza kutoa taarifa kuhusu usaidizi wa janga. Ili kupata kituo cha uokoaji karibu nawe, tembelea DRC Locator (fema.gov) [https://egateway.fema.gov/ESF6/DRCLocator]. Kwa taarifa rasmi kuhusu juhudi za kushughulikia Janga jijini New York, tembelea fema.gov/disaster/4615 [http://www.fema.gov/disaster/4615]. Tufuate kwenye Twitter twitter.com/femaregion2 [http://www.twitter.com/femaregion2] na facebook.com/fema [http://www.facebook.com/fema].