MELEKEZO YA KUKATA RUFAA DHIDI YA UAMUZI WA FEMA [https://www.fema.gov/sw/press-release/20211014/tips-appealing-decision-fema] Release Date: Oktoba 14, 2021 NEW YORK – Ulituma maombi ya msaada wa mikasa wa FEMA baada ya Kimbunga Ida kulikumba Jiji la New York, na ukapokea barua. Huna uhakika barua hiyo inasema nini ila unajua haina habari nzuri.   Mara kwa mara, FEMA hutuma barua hizi wakati ombi lako linakosa habari fulani. Huenda hukutoa vitambulisho vyako, au ithibati ya umiliki wa nyumba husika, au ithibati kwamba uliishi kwenye nyumba hiyo muda mwingi kwa muda kabla ya Kimbunga Ida. Vifuatavyo ni vidokezo vya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa FEMA. Una Siku 60 Kutuma Barua ya Rufaa Yako kwa FEMA Sehemu muhimu zaidi katika mchakato wa rufaa ni kufahamu una muda kiasi gani kutoa mamamiko yako. Hesabu siku 60 kuanzia tarehe ambayo FEMA walifanya uamuzi kwenye barua yao. Hiyo ndiyo tarehe ya kutilia manani ili ikukumbushe kuwa ni siku ya mwisho ya kutuma rufaa yako kwa FEMA. Kumbuka kwamba baada ya FEMA kupokea barua yako, unaweza kupigiwa simu au kutumiwa barua ya ziada ukitakiwa kutoa habari zaidi.   Isome Barua ya FEMA kwa Makini Kabla ya Kuandika Barua Yako Ya Rufaa Utahitajika kufahamu ni kwa nini FEMA walisema maombi yako “hayastahiki,” au kwamba msaada ulioomba umekataliwa, au kwamba FEMA walisitisha kufanya uamuzi kuhusu maombi yako. Mara kwa mara, sababu huenda ikawa ndogo kama vile kukosekana kwa hati au habari fulani. Isome barua ya FEMA kutoka mwanzo hadi mwisho ili uweze kuelewa wanataka ufanye nini. Ambatisha Ushahidi kulifanya Ombi Lako la Rufaa liwe Thabiti Barua yako ya rufaa pekee haitoshi kuwafanya FEMA kubadili uamuzi wao. Unahitaji ushahidi kuunga madai unayotoa kwenye rufaa yako. Ni muhimu kuambatisha hati au habari zilizoombwa na FEMA. Vifuatavyo ni vitu vya kuambatisha na barua yako: * Nakala ya barua ya FEMA iliyokuarifu kwamba maombi yako yamekataliwa, au kwamba FEMA hawakufikia uamuzi.   * BARUA ZA BIMA: Kampuni yako ya bima huenda ilikupa sehemu ndogo tu ya pesa ambayo haikutosha kujenga au kukarabati nyumba yako, haikutosha kukulipia nyumba nyingine, au labda pesa haikutosha kufidia mali yako. Kumbuka kwamba FEMA hawawezi kukupa fedha kwa jambo ambalo tayari limefidiwa na kampuni yako ya bima. * ITHIBATI YA KUISHI KWENYE NYUMBA: Nakala ya stakabadhi ya malipo ya gharama za nyumbani, leseni ya dereva, mkataba au taarifa za benki, stakabadhi za shule iliyo karibu, usajili wa gari au barua ya mwajiri. Hati hizi zote zinaweza kutumika tuthibitisha kwamba nyumba iliyoharibiwa au nyumba ya kupangisha ilikuwa makazi yako ya msingi. “Msingi” kumaanishi uliishi hapo sehemu kubwa ya mwaka.   * ITHIBATI YA UMILIKI: Hati za mkopo au za bima ya nyumba; risiti au stakabadhi ya ushuru; risiti za matengenezo au ukarabati mkubwa za hadi mwaka 2016; au hati za mahakama.  Ikiwa hati zako ziliharibiwa au kupotea, bofya www.usa.gov/replace-vital-documents [http://www.usa.gov/replace-vital-documents] kupata taarifa zaidi jinsi ya kupata hati nyingine.   * RISITI NA MAKIDIRIO: Ambatisha hati za ukarabati wa nyumba, makadirio ya ukarabati, makadirio ya fundi, au taarifa kutoka kwa kampuni yako ya bima.   Ikiwa Huwezi Kuandika Rufaa Yako Mwenyewe, Omba Mtu Mwingine Akuandikie * Ikiwa wewe mwombaji huwezi kuandika rufaa wewe mwenyewe, omba mtu mwingne akuandikie.  Anaweza kuwa mtu wa nyumbani kwako, rafiki au wakili. Waarifu FEMA, katika taarifa iliyotiwa sahihi, kwamba mwandishi ana idhini yako ya kutuma rufaa hiyo kwa niaba yako. Wafanyakazi katika simu ya usaidizi ya FEMA wanaweza kukupa ushauri kuhusu ni nini cha kuambatisha na barua yako ya rufaa na habari kuhusu mambo mengine tofauti na rufaa. * Piga simu kwa NAMBARI YA USAIDIZI YA FEMA 800-621-3362 au simu ya _relay_ ya video (Video Relay Service). Laini za simu hufanya kazi kuanzia saa mbili asubuhi (8 a.m.) hadi saa moja jioni (7 p.m.) siku saba za wiki Barua Yako ya Rufaa Itumwe kwa Njia ya Posta, Faksi au Kupakiwa Mtandaoni; Usisahau Kutia Sahihi na kuandika Tarehe kwenye Barua Yako * Una hadi siku 60 tangu tarehe iliyo kwenye barua ya uamuzi wa FEMA kutuma barua yako ya rufaa kwa njia ya posta, faksi au mtandao ikiwa unataka FEMA wabadili uamuzi wao wa kwanza. Tia sahihi na kuandika tarehe kwenye barua yako ya rufaa. Andika kwenye kila ukurasa nambari ya maombi ya FEMA yenye tarakimu tisa, nambari yako ya mkasa (FEMA-4615-DR-NY), na hati zako za ithibati. * SANDUKU LA POSTA: FEMA National Processing Service Center, P.O. Box 10055, Hyattsville, MD 20782-8055  * FAKSI NAMBA: 800-827-8112, _Attention_: FEMA * Kufungua akaunti ya FEMA mtandaoni au kupakia hati mtandaoni, tembelea www.DisasterAssistance.gov [http://www.disasterassistance.gov/], kisha bofya “Check Status” na kufuata maelekezo. Utarajie Nini Baada ya Kutuma Barua Yako ya Rufaa Ni nini hufuata baada ya kuandika barua yako ya rufaa na kuituma kwenda kwa FEMA ndani ya siku 60 baada ya kupokea barua yao ya uamuzi? Unaweza kupokea simu au barua kutoka kwa FEMA wakiomba taarifa zaidi.  Au FEMA wanaweza kuyafanyia makazi yako ya msingi ukaguzi mwingine. Kwa vyovyote vile, ukishawatumia FEMA barua ya rufaa, waweza kutarajia barua ya uamuzi ndani ya siku 90 baada ya FEMA kupokea barua yako ya rufaa. Kumbuka: * Watu wa kipato cha chini wanaokabiliwa na masuala ya kisheria yaliyotokana na Kimbunga Ida wanaweza kupiga simu isiyokuwa na malipo kupitia 888-399-5459 ili kupata ushauri. Ikiwa unahitaji mtoa huduma ya kisheria awasiliane nawe, Unashauriwa kujaza fomu kupitia https://nysba.org/ida. Mifano ya usaidizi wa kisheria unaopatikana ni pamoja na: * usaidizi wa kupata mafao ya serikali * usaidizi wa madai ya bima ya maisha, afya, na mali * usaidizi kushughulikia mikataba ya ukarabati wa nyumba na ya mafundi * kutayarisha wosia na hati nyingine muhimu za kisheria zilizopotea au kuharibiwa wakati wa kimbunga * masuala ya kumlinda mteja kama vile kupandishwa bei za vitu na kuepuka ulaghai wa mafundi katika mchakato wa kujenga upya * ushauri nasaha kuhusu matatizo ya mkopo wa nyumba * ushauri nasaha kuhusu masuala ya mpangangaji na mwenye nyumba * Ni muhimu kufahamu kwamba msaada wa FEMA si kibadala cha bima na hauwezi kufidia hasara zote zilizosababishwa na mkasa fulani; msaada wa FEMA unalenga kugharamia mahitaji ya kimsingi na kupiga jeki tu juhudi nyingine za kushughulikia mkasa.  * Unaweza kutuma maombi ya Usaidizi wa FEMA kwa: Kembelea DisasterAssistance.gov [http://www.disasterassistance.gov/], kutumia program tumizi ya simu ya FEMA au kupiga simu NAMBARI YA USAIDIZI YA FEMA 800-621-3362 (VRS). Laini za simu hufanya kazi kuanzia saa mbili asubuhi (8 a.m.) hadi saa moja jioni (7 p.m.) siku saba za wiki, na wahudumu wanaweza kukuunganisha na mtaalamu anayezungumza lugha yako. * Ikiwa unatumia huduma ya simu ya wasiosikia/walemavu (relay call) kama vile huduma ya _relay_ ya video (VRS), huduma ya simu ya maandishi (captioned telephone) au huduma nyingine, wape FEMA nambari ya huduma hiyo. * Unaweza kutembelea Kituo cha Kushughuliki Waathiriwa wa Mikasa na kukutana ana kwa ana na wafanyakazi wa FEMA na wawakilishi wengine wa mashirika ya kitaifa na jimbo ambao wanaweza kukupa taarifa zaidi kuhusu misaada ya mikasa.  Kupata kituo cha kushughulikia waathiriwa wa mikasa karibu nawe, tembelea DRC Locator (fema.gov) [https://egateway.fema.gov/ESF6/DRCLocator]. * SIKU YA MWISHO YA KUTUMA MAOMBI YA MISAADA YA MIKASA YA FEMA NI JUMATATU, DISEMBA, 6. * Kupata habari zaidi mtandaoni pamoja na vijitabu vya FEMA vinavyoweza kupakuliwa, tembelea DisasterAssistance.gov [http://www.disasterassistance.gov/] kisha ubofye _“Information.”_ * Kwa rufaa kwenda kwa mashirika yanayosaidia katika mahitaji mahususi ya jamii, piga simu 211 au temebelea https://www.211nys.org/contact-us. Kwa wakazi wa mji wa York City, piga simu 311. * Kwa taarifa za hivi karibuni kuhusu juhudi za kutoa misaada kwa waathiriwa wa Kimbunga Ida, tembelea fema.gov/disaster/4615 [http://www.fema.gov/disaster/4615]. Fuatilia taarifa zetu kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii kupitia twitter.com/femaregion2 [http://www.twitter.com/femaregion2] and facebook.com/fema [http://www.facebook.com/fema].