JITAHADHARI NA MATAPELI NA WALAGHAI [https://www.fema.gov/sw/fact-sheet/beware-fraud-and-scam-artists-2] Release Date: Oct 4, 2021 Baada ya mkasa, walaghai, matapeli na wahalifu wengine mara nyingi hujitokeza kuwahadaa waathiriwa wa mkasa.  Maafisa wa kitaifa na wa jimbo wanaosimiamia majanga ya dharura wanawasihi wakazi kuwa makini na kuripoti vitendo vyovyote vya kutiliwa shaka. Walaghai wanaweza kuwadanganya waathiriwa kwa kujifanya wasaidizi rasmi wakati  wa mikasa au hata kwamba wao ni jamaa za waathiriwa wanaojaribu kuwasaidia waathiriwa kufanya maombi ya msaada. Utapeli wa mara kwa mara unaoripotiwa baada ya mikasa ni pamoja na: MISAADA BANDIA YA KITAIFA AU JIMBO: Wafanyakazi wa kitaifa au jimbo hawaombi au kupokea pesa.  Wafanyakazi wa FEMA pamoja na wale wa Usimamizi wa Biashara Ndogo Ndogo wa Marekani hawalipishi kitu kwa wanaoomba msaada wa mikasa, ukaguzi au usaidizi wa kufanya maombi. WAKAGUZI BANDIA WA MAKAZI: Mkasa ukitokea, waombaji msaada wanaweza kujikuta wakihadaiwa na wakaguzi bandia wa makazi wanaodai kuwa wawakilishi wa FEMA wanaokadiria hasara iliyotokea. Sisitiza uonyeshwe kitambulisho cha mkaguzi. Wafanyakazi wote wa FEMA wanakuwa na kitambulisho cha picha kilichojaladiwa. Wakaguzi wa makazi huwa na nambari ya usajili ya FEMA ya kila mwombaji yenye dijiti tisa.  Wakaguzi wa nyanjani wanaweza kutumia aina mbalimbali za mawasiliano kuwasiliana na waombaji misaada. Wakaguzi wanaweza kutumia simu walizopewa na serikali au simu zao za kibinafsi hivyo waombaji wanaweza kupokea simu zenye kodi za maeneo mbalimbali. Wakaguzi aidha wanaweza kuwasiliana kwa arafa au barua pepe wakitumia njia za mawasiliano zilizopeanwa na mwombaji kwenye fomu ya FEMA. Hata hivyo, wakaguzi hawaombi pesa ili wafanye ukaguzi. Kuna wakati ambapo wawakilishi wa FEMA wanaweza kuwasiliana nawe kuthibitisha habari zako za kibinafsi. Katika hali hiyo unapaswa kuwauliza nambari yao ya utambulisho ya FEMA.  Ikiwa huna uhakika na utambulisho wa anayewasiliana nawe au unashuku mtu anayesema yeye ni mkaguzi wa makazi aliyetumwa na FEMA, piga simu kwa NAMBARI HII YA MSAADA YA FEMA 800-621-3362 (711/VRS). Laini za simu hufanya kazi kuanzia saa mbili asubuhi (8 a.m.) hadi saa moja jioni (7 p.m.) siku saba za wiki, na wahudumu wanaweza kukuunganisha na mtaalamu anayezungumza lugha yako. Ikiwa unatumia nambari au laini ya simu ya _wasiosikia/walemavu (relay call) _kama vile huduma ya _relay_ ya video, huduma ya simu ya maandishi (captioned telephone) au huduma nyingine, wape FEMA nambari ya huduma hiyo. WAFANYAKAZI BANDIA WA SERIKALI: Unaweza kupokea mawasiliano kutoka kwa matapeli wanaojifanya wafanyakazi wa mikasa wanaoomba pesa ili kutoa huduma. Wafanyakazi wa kitaifa, jimbo au mtaa hawaombi au kupokea pesa. Wala wafanyakazi wa mikasa wa kitaifa hawatoi ahadi ya kupata ruzuku ya mkasa. MASHIRIKA YA UONGO YA MISAADA: Orodha ya mashirika ya misaada yanayoaminika na yaliyoidhinishwa na Muungano wa _Wise Giving_ wa _Better Business Bureau_ inapatikana hapa Give.org [http://www.give.org/]. Wahalifu huwahadaa waathiriwa kwa kutuma ujumbe wa kutapeli kupitia barua pepe au mitandao ya kijamii na kwa kuunda wavuti bandia kwa nia ya kuomba michango. Muungano wa _Wise Giving_ unakushauri kwamba: “Usijibu barua pepe ambazo hukutarajia wala kuzifahamu. Jitahadhari dhidi ya wauzaji kwa njia ya simu na mashirika bandia ya misaada yanayoonekana kuwa halisi kwa kutumia majina yanayokaribia kufanana na mashirika halisi.” Kwa taarifa zaidi kuhusu jinsi ya kuepukana na mashirika bandia ya misaada, tembelea wavuti ya Kamisheni ya Biashara ya Kitaifa (Federal Trade Commission) kupitia Scam Alerts [https://usfema-my.sharepoint.com/personal/0376056852_fema_dhs_gov/Documents/Documents/00-4615%20NEW%20YORK/4615%20Products/Fact%20Sheets/Scam%20Alerts]. UTAPELI KWA NJIA YA MATANGAZO YA NYUMBA ZA KUPANGA: Kamisheni ya Biashara ya Kitaifa (Federal Trade Commission) ina taarifa jinsi utapeli kwa njia ya matangazo ya nyumba za kupanga hufanya kazi. Kwa mfano, watapeli wanafahamu kwamba huwa vigumu sana kupata nyumba za kupanga hivyo pendekezo linalovutia ni vigumu likataliwe. Jifunze zaidi katika Rental Listing Scams [https://usfema-my.sharepoint.com/personal/0376056852_fema_dhs_gov/Documents/Documents/00-4615%20NEW%20YORK/4615%20Products/Fact%20Sheets/Rental%20Listing%20Scams]. CHUKU TAHADHARI DHIDI YA MAFUNDI WASIOKUWA NA LESENI/BIMA: Mara nyingi baada ya mkasa, watu watajitokeza kama mafundi halali. Waombe marejeleo yao, chukua tahadhari na malipo unayotoa, na uhakikishe wana leseni na kupata vibali mwafaka.  Kabla ya kuingia mkataba na fundi wa nyumba, thibitisha kwamba fundi huyo ana leseni au amesajiliwa katika kaunti yako: * JIJI LA NEW YORK: https://www1.nyc.gov/site/dca/consumers/check-license.page     * KAUNTI YA NASSAU: Licensing / Registrations | Nassau County, NY - Official Website (nassaucountyny.gov) [https://www.nassaucountyny.gov/1563/Licensing-Registrations] * KAUNTI YA SUFFOLK: https://www.suffolkcountyny.gov/Departments/Consumer-Affairs * KAUNTI YA ROCKLAND: http://rocklandgov.com/departments/consumer-protection-weights-and-measures/licensed-businesses * KAUNTI YA WESTCHESTER: https://consumer.westchestergov.com/trades/find-a-licensed-contractor Ukiwa na taarifa ya ulaghai, au matumizi mabaya ya raslimali, unaweza kuripoti—saa 24 za siku, siku saba za wiki— kupitia kwa Nambari ya Dharura ya FEMA ya kuripoti ulaghai 866-720-5721 au barua pepe Disaster@leo.gov. Ukijua kwamba wewe au mpendwa wako amelaghaiwa au amekuwa mhanga wa utapeli, piga ripoti mara moja katika kituo cha polisi kilicho karibu nawe au katika idara ya _sherifu_, au wasiliana na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Jimbo la New York: * Nambari ya Dharura ya Kuwakinga Wateja, 800-697-1220 * https://www.ny.gov/agencies/division-consumer-protection * https://dos.ny.gov/file-consumer-complaint Kwa rufaa kwenda kwa mashirika yanayosaidia katika mahitaji mahususi ya jamii, piga simu 211 au temebelea https://www.211nys.org/contact-us. Kwa wakazi wa Jiji la York City, piga simu 311. Kwa taarifa za hivi karibuni kuhusu juhudi za mutoa misaada kwa waathiriwa wa Kimbunga Ida, tembelea fema.gov/disaster/4615 [http://www.fema.gov/disaster/4615]. Fuatilia taarifa zetu kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii kupitia twitter.com/femaregion2 [http://www.twitter.com/femaregion2] and facebook.com/fema [http://www.facebook.com/fema].