FEMA Inaandaa Njia Nyingi za Kuunganisha Walionusurika

Release Date Release Number
009
Release Date:
Julai 27, 2023

WILLISTON, VT – Pesa za serikali zinapatikana kwa watu walioathiriwa ambao nyumba zao au mali ya kibinafsi ziliharibiwa na dhoruba kali za Julai, mafuriko, maporomoko ya ardhi na maporomoko ya matope katika kaunti tisa: Caledonia, Chittenden, Lamoille, Orange, Orleans, Rutland, Washington, Windham na Windsor.

FEMA iko katika jamii, inawapa walionusurika njia nyingi za kutuma maombi ya msaada na kufanya kazi na mwakilishi wa FEMA kuhusu kesi yao.

Jinsi ya kutuma maombi:

Kuomba msaada wa majanga, waathirika wanaweza:

 • Kutembelea DisasterAssistance.gov;
 • Kupakua FEMA mobile app kutoka Apple App Store au Google Play Store; 
 • Piga simu kwa laini isiyolipishwa ya FEMA kwa 800-621-3362, inafunguliwa saa moja asubuhi (7 a.m) hadi saa tano usiku (11 p.m) Masaa ya mashariki na tafsiri ya lugha ya inapatikana. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji kama vile huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au huduma zingine, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo unapotuma ombi; au
 • Ungana na FEMA ana kwa ana katika Kituo cha Msaada wa Majanga, Kituo cha Kusaidia Biashara, katika jamii yako ya kuenda nyumba kwa nyumba na katika Vituo vya Rasilimali vya Mashirika mengi vilivyo katika eneo lote lililoathiriwa.

Vituo vya Msaada wa Majanga (DRC)

Vituo vya Msaada wa Majanga hutoa usaidizi wa ana kwa ana kwa watu binafsi na wamiliki wa biashara ndogo. Wataalamu wa urejeshi kutoka FEMA, Usimamizi wa Biashara Ndogo ya Marekani (SBA), na rasilimali za ziada zinapatikana ili kuwasaidia walionusurika.

 • Vituo viwili vya Msaada wa Majanga vimefunguliwa katika kaunti za Rutland na Washington. Maeneo hayo ni:
  • ASA Bloomer Building, 88 Merchants Row, Rutland, VT 05701 
  • Waterbury Armory, 294 Armory Drive, Waterbury, VT 05676
  • Barre Auditorium, 16 Auditorium Hill, Barre, VT 05641
  • Flood Brook School, 91 Vermont – 11, Londonderry, VT 05148

Maeneo ya ziada yatatangazwa yanapoanza kufanya kazi. Maeneo na saa za kazi za DRC zinaweza kupatikana hapa DRC Locator (fema.gov/drc).

Vituo vinaweza:

 • Kutoa msaada wa kujaza maombi;
 • Kusasisha hali ya maombi ya aliyenusurika;
 • Saidia kuwasilisha hati za ziada kwa FEMA;
 • Kutoa huduma za rufaa kwa mashirika ya kujitolea yanayotoa huduma mbalimbali kwa waathirika; na
 • Kuwezesha kupatika kwa msaada wa mkopo na huduma ya wateja ya Usimamizi wa Biashara Ndogo ya Marekani.

 Vituo vya Rasilimali ya Mawakala (MARCs):

MARC ni eneo moja ambapo mashirika ya umma na ya kibinafsi hukusanyika ili kusaidia wale walioathiriwa na majanga. MARCs ni shughuli shirikishi.

Maeneo na saa za kazi zinaweza kupatikana: https://vem.vermont.gov/flood/marc

Msaada kwa Waathirika wa Majanga (DSA):

Timu za DSA kutoka FEMA zinaenda nyumba kwa nyumba katika jamii za Vermont, kuzuru vitongoji na kusaidia wakazi walioathiriwa na dhoruba kutuma maombi ya msaada wa majanga ya FEMA.

Wafanyakazi wa DSA wanatembelea nyumba, shule, mashirika yasiyo ya kibiashara na jamii ambazo hazifikiki kwa urahisi. Pia wanakutana na viongozi wa mitaa na viongozi wa jamii ili kubaini masuala yanayohusiana na majanga na mahitaji ambayo hayajatimizwa.

Timu za DSA zinaweza kuwasaidia walionusurika kutuma maombi ya usaidizi, kusasisha maelezo yao na kusaidia na marejeleo kwa washirika wa wakala wa kujitolea. Wanaweza kuwapa wakaaji fursa ya kutumia kompyuta ya mkononi kujiandikisha au kujitolea kuingiza habari kwa niaba yao. Wafanyakazi wa DSA huvaa beji ya utambulisho ya FEMA pamoja na picha zao.

Usimamizi wa Biashara Ndogo za Marekani (SBA):

SBA imefungua Vituo vya Kusaidia Biashara (BRCs) katika maeneo matatu ili kuwasaidia wamiliki wa nyumba, wapangaji, biashara za ukubwa wote na mashirika yasiyo ya kibiashara ambayo yanahitaji usaidizi wa kutuma maombi ya mkopo wa muda mrefu wa majanga wa SBA yenye riba nafuu:

 • Kauni ya Washington: 751 Granger Road Berlin, Vermont 05641 
 • Kaunti ya Windsor: 126 Main Street Ludlow, Vermont 05149 
 • Kaunti ya Lamoille: 29 Sunset Drive, Morrisville, VT 05661

visit Kwa maeneo na saa za kazi tafadhali tembelea: https://www.sba.gov/article/2023/07/17/sba-offers-disaster-assistance-businesses-residents-vermont-affected-recent-severe-storms-flooding

Ikiwa unaishi katika kaunti ambayo haijateuliwa na ulipata uharibifu unaweza kupiga Simu kwa Laini ya Usaidizi ya FEMA kwa 1-800-621-3362 ili kutuma ombi na uteuzi wa kaunti yako ukitokea, ombi lako litaanza kushughulikiwa.

Kwa habari za hivi punde tembelea fema.gov/disaster/4720. Fuata akaunti ya  Region 1 katika Twitter twitter.com/FEMARegion1 au ukurasa wa Facebook kwa facebook.com/FEMA.

Kwa masasisho kuhusu majibu na msaada wa Vermont, fuata Wakala wa Usimamizi wa Dharura wa Vermont twitter.com/vemvt kwenye Twitter na Facebook facebook.com/vermontemergencymanagement

FEMA imejitolea kuhakikisha msaada wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa majanga au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wa lugha mbali mbali wanapatikana

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho