Wafanyakazi wa FEMA wa Kusaidia Walionusurika Majanga Wanategemeza Jamii za Vermont

Release Date Release Number
010
Release Date:
Julai 27, 2023

Timu za Kusaidia Walionusurika Majanga (DSA) kutoka FEMA zinaenda nyumba kwa nyumba katika jamii za Vermont, kuzuru vitongoji na kusaidia wakazi walioathiriwa na mafuriko kujiandikisha kwa msaada wa FEMA wa majanga.

Wafanyakazi wa DSA wanatembelea nyumba, shule, mashirika yasiyo ya kibiashara na jamii ambazo hazifikiki kwa urahisi. Pia wanakutana na viongozi wa mitaa na viongozi wa jamii ili kubaini masuala yanayohusiana na majanga na mahitaji ambayo hayajatimizwa.

Timu za DSA zinaweza kuwasaidia walionusurika kujiandikisha kwa msaada, kusasisha maelezo yao na kusaidia kwa marejeleo kwa washirika wa wakala wa kujitolea. Wanaweza kuwapa wakaaji fursa ya kutumia kompyuta kibao kujiandikisha au kujitolea kuandika habari kwa niaba yao.

Wafanyakazi wa DSA hawatawahi kuomba au kukubali pesa. Wafanyakazi wa DSA huvaa beji ya utambulisho wa FEMA yenye picha - shati, fulana au koti ya FEMA si uthibitisho wa utambulisho. Wakati wa kumsaidia mtu kujiandikisha, anaweza kuuliza habari za kibinafsi, ikijumuisha nambari ya ruzuku ya jamii, mapato ya mwaka na taarifa za benki. Wakazi wanahimizwa kuitisha kitambulisho kabla ya kutoa habari yoyote ya kibinafsi.

Watu walioathiriwa na mafuriko katika kaunti za Caledonia, Chittenden, Lamoille, Orange, Orleans, Rutland, Washington, Windham na Windsor hawahitaji kusubiri wafanyakazi wa DSA kujiandikisha ili kupata usaidizi. Ili kujisajili pakua FEMA Mobile App,tembelea DisasterAssistance.gov, au piga simu kwa 1-800-621-3362. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo unapotuma ombi.

FEMA imejitolea kuhakikisha msaada wa majanga unatekelezwa kwa usawa, bila ubaguzi kwa misingi ya rangi, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi. Mwathiriwa yeyote wa majanga au mwananchi anaweza kuwasiliana na Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA ikiwa anahisi kuwa ameathiriwa na ubaguzi. Ofisi ya Haki za Kiraia ya FEMA inaweza kupatikana bila malipo kwa 833-285-7448. Maopareta wanaotumia lugha mbali mbali wanapatikana.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho