Kituo cha Msaada wa Majanga cha FEMA kilicho St. Louis Kitafungwa tarehe 7 Novemba

Release Date Release Number
25
Release Date:
Novemba 1, 2022

Kituo cha Msaada wa Majanga (DRC) katika Chuo cha Ufundi cha Ranken huko St. Louis kitafungwa Jumatatu, Novemba 7 saa kumi na moja jioni (5pm).Tarehe 7 Novemba pia ni tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ya usaidizi wa serikali kwa watu binafsi huko St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles iliyoathiriwa moja kwa moja na dhoruba na mafuriko ya Julai 25-28.
 

Ranken Technical College

Mary Ann Lee Technology Center

1313 N. Newstead Ave.

St. Louis, MO 63113

(Kona ya Newstead na Page)

Itafungwa kabisa Jumatatu, Novemba 7 saa kumi na moja jioni (5 p.m.)


Pamoja na kutuma maombi ya usaidizi katika DRC, kuna njia kadhaa kwa wapangaji na wamiliki wa nyumba ambao waliathiriwa na dhoruba na mafuriko za Julai kuomba usaidizi wa majanga wa FEMA kabla ya tarehe ya mwisho ya Novemba 7.

  • Ikiwa unatumia huduma ya kupitisha ujumbe, kama vile kupitisha ujumbe kupitia video (VRS), simu iliyo na maelezo mafupi au huduma nyingine, pea FEMA nambari ya huduma hiyo. Nambari ya Msaada inafunguliwa siku saba kwa wiki. Bonyeza 2 kwa Kihispania au 3 ili kupata mkalimani anayezungumza lugha yako.

Usaidizi wa kisheria bila malipo unapatikana kwa watu binafsi katika St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles wanaohitaji usaidizi kuhusu masuala yanayohusiana na mafuriko, kama vile mikataba ya ukarabati wa nyumba na madai ya bima, masuala ya mwenye nyumba na kubadilisha hati za kisheria.

Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA na @FEMARegion7.

Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov na FEMA.gov/disaster/4665.

Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho