Kituo cha Msaada wa Majanga huko Hazelwood Kitafungwa Wiki Ijayo na Kitafunguliwa Tena kama Kituo cha Kutoa Mikopo ya Majanga.

Release Date Release Number
18
Release Date:
Oktoba 6, 2022

Kituo cha Msaada wa Majanga katika Kaunti ya St. Louis kitafungwa Jumatano, Oktoba 12 saa kumi na mbili jioni (6 p.m). Kitafunguliwa tena kama Kituo cha Kutoa Mikopo ya Majanga (DLOC)  cha Utawala wa Biashara Ndogo ya Marekani (SBA) mnamo Alhamisi, Oktoba 13 saa tatu asubuhi (9 a.m).

Kituo cha Hazelwood Civic

8969 Dunn Road

Hazelwood, MO 63042

DLOC zitakuwa na wawakilishi wa huduma kwa wateja ili wakutane na wafanyabiashara na wakazi kutoka Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles, ambao waliathiriwa na mafuriko na dhoruba kali iliyotokea Julai 25–28 Julai 2022. Wawakilishi wa SBA watajibu maswali, wataeleza programu yao ya mkopo wa maafa na kukamilisha mikopo ya wateja iliyoidhinishwa ya majanga kwa siku na nyakati zilizoonyeshwa. Hakuna miadi inahitajika.

Vituo vingine vya Kutoa Mikopo ya Majanga vinapatikana katika:

Kituo cha Manispaa ya O’Fallon

Kiingilio cha Kusini-mashariki

100 N Main St.

O’Fallon, MO 63366

Kituo cha Salvation Army Temple

(Karibu na kona ya Arsenal na California)

2740 Arsenal St

St. Louis, MO 63118      

Masaa: Jumatatu– Ijumaa, saa tatu asubuhi hadi (9 a.m.)– saa kumi na mbili jioni (6 p.m.)

Vituo vitatu vya Msaada wa Majanga vitasalia wazi ili kuwasaidia waathiriwa walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko ya Julai 25-28 na dhoruba kali:

JIJI LA ST. LOUIS

Chuo cha Ranken Technical

Kituo cha Teknolojia cha Mary Ann Lee

1313 N. Newstead Ave.

St. Louis, MO 63113

(Kwenye kona ya Newstead na Page)

KAUNTI YA ST. LOUIS

Kituo cha Urban League Empowerment

9420 W. Florissant Ave.

Ferguson, MO 63136


Kituo cha University City Recreation

Centennial Commons

7210 Olive Blvd.

University City, MO 63130

Masaa ya vituo vya Msaada:

Jumatatu – Ijumaa, saa mbili asubuhi (8 a.m.)– saa kumi na mbili jioni (6 p.m.)

Jumamosi, saa mbili asubuhi (8 a.m.) – saa kumi na moja (5 p.m.)

Inafungwa Jumapili

Katika vituo vya msaada wataalamu kutoka FEMA na Usimamizi wa Biashara Ndogo za Marekani wanatoa taarifa kuhusu huduma zinazopatikana, kueleza mipango ya usaidizi na kuwasaidia walionusurika kukamilisha au kuangalia hali ya maombi yao.

  • Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ya FEMA ni Oktoba 7.
     
  • Tuma ombi kwa FEMA mtandaoni kupitia DisasterAssistance.gov au piga simu kwa 800-621-FEMA (3362).
     
  • Iwapo unahitaji usaidizi kutuma ombi, FEMA inaweza kukusaidia katika Kituo cha Msaada wa Majanga.
     
  • Hakuna miadi inahitajika kutembelea Kituo cha Msaada wa Majanga. Wanaokuja bila miadi wanakaribishwa.
  • Watu walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko katika Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles wanaweza kutembelea kituo chochote cha msaada kupata usaidizi wa ana kwa ana.        

Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA na @FEMARegion7.

Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov na FEMA.gov/disaster/4665.

Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho