Kituo kipya cha Msaada wa Majanga cha FEMA kitafunguliwa Jumamosi, Septemba 10, katika Jiji la St. Louis ili kutoa usaidizi wa ana kwa ana kwa watu walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko ya Julai 25—28 na dhoruba kali.
Wataalamu wa Misaada kutoka FEMA na Usimamizi wa Biashara Ndogo za Marekani watatoa taarifa kuhusu huduma zinazopatikana, kueleza mipango ya usaidizi na kuwasaidia walionusurika kukamilisha au kuangalia hali ya maombi yao.
Vituo vya msaada wa majanga vinapatikana katika:
Kituo cha Salvation Army Temple
2740 Arsenal St
St. Louis, MO 63118
(Karibu na kona ya Arsenal na California)
Masaa ya jumamosi: saa mbili asubuhi (8 a.m.) – saa kumi na moja jioni (5 p.m.)
Kuanzia Jumatatu, Septemba 12, masaa mapya za vituo vyote vya msaada itakuwa:
Jumatatu – Ijumaa, saa mbili asubuhi (8 a.m.) – saa kumi na mbili jioni (6 p.m).
Jumamosi, saa mbili asubuhi (8 a.m.) – saa kumi na moja jioni (5 p.m.)
Inafungwa Jumapili
Vituo vingine vya msaada vimefunguliwa katika maeneo haya:
JIJI LA ST. LOUIS
Chuo cha Ranken Technical
Kituo cha Teknolojia cha Mary Ann Lee
1313 N. Newstead Ave.
St. Louis, MO 63113
(Kwenye kona ya Newstead na Page)
KAUNTI YA ST. LOUIS
Kituo cha Urban League Empowerment
9420 W. Florissant Ave.
Ferguson, MO 63136
Kituo cha University City Recreation
Centennial Commons
7210 Olive Blvd.
University City, MO 63130
Kituo Hazelwood Civic
8969 Dunn Road
Hazelwood, MO 63042
KAUNTI YA ST. CHARLES
Kituo cha Manispaa ya O’Fallon
100 N. Main St.
O’Fallon, MO 63366
(Kiingilio cha Kusini-mashariki)
Bodi ya Rasilimali za Ulemavu Unaoendelea – Jengo la DDRB
1025 Country Club Road
St. Charles, MO 63303
(I-70 karibu na njia ya kutoka Zumbehl)
Eneo la DDRB litafungwa kabisa Jumatano, Septemba 14, saa kumi na mbili jioni (6pm).
Hakuna miadi inahitajika kutembelea Kituo cha Msaada wa Majanga. Wanaokuja bila miadi wanakaribishwa
Watu walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko katika Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles wanaweza kutembelea kituo chochote cha msaada.
Ikiwa unahitaji msaada kutuma maombi, FEMA inaweza kukusaidia katika Kituo cha Msaada wa Majanga.
Tuma ombi na FEMA mtandaoni kwenye DisasterAssistance.gov au piga simu 800-621-FEMA (3362).
FEMA inaweza kutoa pesa za ruzuku ya Usaidizi wa Mtu Binafsi ambazo si lazima zilipwe kwa:
- Msaada wa Kodi ya Nyumba ikiwa unahitaji kuhama kwa sababu ya uharibifu wa mafuriko
- Mali ya kibinafsi ambayo iliharibika au kuharibiwa na mafuriko
- Kurudishiwa Malipo ya Mahali pa kulala ikiwa ulilazimika kukaa katika hoteli kwa muda
- Marekebisho ya Msingi ya Nyumba kwa wamiliki wa nyumba ambao makazi yao ya msingi yaliharibiwa na mafuriko
- Mahitaji Mengine Muhimu yaliyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni
Mbali na msaada ulioorodheshwa, tafadhali kumbuka yafuatayo:
- Ombi moja tu kwa kila familia
- FEMA hailipii chakula kilichopotea au kuharibika
- Kisheria, Fema hairuhusiwi kulipia tena malipo ya bima au usaidizi uliotolewa na vyanzo vingine
Wamiliki wa Nyumba na Wapangaji: Baada ya kutuma maombi na FEMA Ikiwa umetumwa kwa SBA kwa ajili ya mkopo wa majanga, tafadhali wasilisha ombi. Kuwasilisha ombi la SBA hukuwezesha kuzingatiwa kwa ajili ya ruzuku za ziada ikiwa utanyimwa mkopo wa SBA.
Ikiwa unastahili kupata mkopo, utakuwa na rasilimali hiyo ikiwa utachagua kuikubali.
Usaidizi wa ombi lako la SBA unapatikana katika Vituo vyovyote vya Msaada wa Majanga.
Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA na @FEMARegion7.
Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov na FEMA.gov/disaster/4665.
Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi.