Kituo cha Msaada wa Majanga Kinafunguliwa katika O’Fallon, Missouri

Release Date Release Number
010
Release Date:
August 31, 2022

Kituo cha msaada wa majanga cha FEMA kitafunguliwa katika O’Fallon, Missouri (Kaunti ya St. Charles) mnamo Alhamisi, Septemba 1 ili kutoa usaidizi wa moja kwa moja kwa watu walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko na dhoruba kali Julai 25—28.

Wataalamu wa Misaada kutoka FEMA na Usimamizi wa Biashara Ndogo Marekani watatoa taarifa kuhusu huduma zinazopatikana, kueleza mipango ya usaidizi na kuwasaidia walionusurika kukamilisha au kuangalia hali ya maombi yao.

Kituo cha msaada wa majanga kinapatikana katika:

Kituo cha Manispaa ya O'Fallon

100 N. Main St.

O’Fallon, MO 63366

(Kiingilio cha Kusini-mashariki)

SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.)

  • Baada ya Jumapili hii, Septemba 4, Vituo vyote sita vya Msaada wa Majanga vya FEMA vitakuwa vinafungwa Jumapili.
  • Vituo vya Msaada wa Majanga bado vitafunguliwa siku sita kwa wiki: Jumatatu-Jumamosi saa Mbili asubuhi (8 a.m.)–saa Moja jioni (7 p.m.) hadi notisi nyingine itolewe
  • Saa za Siku ya Wafanyikazi: Vituo vyote vya Msaada wa Majanga vitafunguliwa saa Mbili asubuhi (8 a.m.) hadi saa Moja jioni (7 p.m.). Siku ya Wafanyakazi, Jumatatu, Septemba 5

Vituo vingine vya msaada vimefunguliwa katika:

KAUNTI YA ST. LOUIS

Kituo cha Urban League Empowerment                       

9420 W Florissant Ave.

Ferguson, MO 63136

SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.).

KAUNTI YA ST. LOUIS

Kituo cha University City Recreation

Centennial Commons

7210 Olive Blvd

University City, MO 63130

SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.)

KAUNTI YA ST. LOUIS

Kituo cha Hazelwood Civic

8969 Dunn Road

Hazelwood, MO 63042                                   

SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.).

JIJI LA ST. LOUIS

Chuo cha Ranken Technical

Kituo cha Teknolojia cha Mary Ann Lee

1313 N. Newstead Ave.

St. Louis, MO 63113

(Kwenye kona ya Newstead na Page)

SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.)

KAUNTI YA ST. CHARLES

Bodi ya Rasilimali za Ulemavu Unaoendelea – Jengo la DDRB

1025 Country Club Road

St. Charles, MO 63303

(I-70 karibu na njia ya kutoka Zumbehl)

SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.).

Hakuna miadi inahitajika kutembelea Kituo cha Msaada wa Majanga. Wanaokuja bila miadi wanakaribishwa.

Kabla ya kutembelea kituo, tuma ombi na FEMA mtandaoni kwenye DisasterAssistance.gov au piga simu 800-621-FEMA (3362).

Saa za Siku ya Wafanyikazi:  Saa Mbili asubuhi (8 a.m.) hadi Saa Kumi na moja jioni (5 p.m.)

Watu walioathiriwa moja kwa moja na mafuriko katika Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles wanaweza kutembelea kituo chochote cha msaada.

Kwa mahitaji yanayohusiana moja kwa moja na mafuriko ya Julai 25—28, FEMA inaweza kutoa pesa za ruzuku ya Usaidizi wa Mtu Binafsi ambazo si lazima zilipwe kwa:

  • Msaada wa Kodi ya Nyumba ikiwa unahitaji kuhama kwa sababu ya uharibifu wa mafuriko
  • Mali ya kibinafsi ambayo iliharibika au kuharibiwa na mafuriko
  • Kurudishiwa Malipo ya Mahali pa kulala ikiwa ulilazimika kukaa katika hoteli kwa muda
  • Marekebisho ya Msingi ya Nyumba kwa wamiliki wa nyumba ambao makazi yao ya msingi yaliharibiwa na mafuriko
  • Mahitaji Mengine Muhimu yaliyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni

Mbali na msaada ulioorodheshwa, tafadhali kumbuka yafuatayo:

  • Ombi moja tu kwa kila familia
  • FEMA hailipii chakula kilichopotea au kuharibika

Kisheria. Fema hairuhusiwi kulipia tena malipo ya bima au usaidizi uliotolewa na vyanzo vingine.                    

Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA na @FEMARegion7.

Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov na FEMA.gov/disaster/4665.

Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi.

Tags:
Last updated September 1, 2022