Dola Milioni 33 Zaidhinishwa kwa Wakazi wa Eneo la St. Louis Katika Mwezi wa Kwanza Baada ya Mafuriko

Release Date Release Number
007
Release Date:
Agosti 24, 2022

Mwezi mmoja baada ya mafuriko yaliyorekodiwa kupiga eneo la St. Louis huko Missouri, zaidi ya dola milioni 33 zimeidhinishwa kuwasaidia walionusurika kurejealea hali ya kawaida.

Vituo Vitatu vya Msaada wa Majanga Hufunguliwa Siku 7 kwa Wiki kwa Usaidizi wa Moja kwa Moja

KAUNTI YA ST. LOUIS

Kituo cha Hazelwood Civic

8969 Dunn Road

Hazelwood, MO 63042                                   

SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.) siku saba kwa wiki hadi notisi nyingine itolewe

JIJI LA ST. LOUIS

Chuo cha Ranken Technical

Kituo cha Teknolojia cha Mary Ann Lee

1313 N. Newstead Ave.

St. Louis, MO 63113

(Kwenye kona ya Newstead na Page)

SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.) siku saba kwa wiki hadi notisi nyingine itolewe

KAUNTI YA ST. CHARLES

Bodi ya Rasilimali za Ulemavu Unaoendelea – Jengo la DDRB

1025 Country Club Road

St. Charles, MO 63303

(I-70 karibu na njia ya kutoka Zumbehl)

SAA: Mbili asubuhi (8 a.m.)–Moja jioni (7 p.m.) siku saba kwa wiki hadi notisi nyingine itolewe

Hakuna miadi inahitajika kutembelea Kituo cha Msaada wa Majanga. Wanaokuja bila miadi wanakaribishwa.

Kabla ya kutembelea kituo, tuma ombi na FEMA mtandaoni kwenye DisasterAssistance.gov au piga simu 800-621-FEMA (3362).

Kwa mahitaji ambayo hayajashughulikiwa na bima au vyanzo vingine, FEMA inaweza kutoa usaidizi wa pesa kwa Mtu Binafsi ambazo si lazima zilipwe kwa:

  • Msaada wa Kodi ya Nyumba ikiwa unahitaji kuhama kwa sababu ya uharibifu wa mafuriko
  • Mali ya kibinafsi ambayo iliharibika au kuharibiwa na mafuriko
  • Kurudishiwa Malipo ya Mahali pa kulala ikiwa ulilazimika kukaa katika hoteli kwa muda
  • Marekebisho ya Msingi ya Nyumba kwa wamiliki wa nyumba ambao makazi yao ya msingi yaliharibiwa na mafuriko
  • Mahitaji Mengine Muhimu yaliyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni

Mbali na msaada ulioorodheshwa, tafadhali kumbuka yafuatayo:

  • Ombi moja tu kwa kila familia
  • FEMA hailipii chakula kilichopotea au kuharibika
  • Kisheria, FEMA hairuhusiwi kulipia tena malipo ya bima au usaidizi uliotolewa na vyanzo vingine

Wamiliki wa Nyumba na Wapangaji: Ikiwa umetumwa kwa SBA kwa mkopo wa majanga, tafadhali wasilisha ombi. Kuwasilisha ombi la SBA hukuwezesha kuzingatiwa kwa ruzuku za ziada. Ikiwa unastahili kupata mkopo, utakuwa na rasilimali hiyo ikiwa utachagua kuikubali.
 

Tafadhali Wasiliana na FEMA

  • Ikiwa uliathiriwa moja kwa moja na mafuriko - na una mahitaji ambayo hayajatimizwa - tafadhali wasiliana.
  • Tafadhali ambia FEMA kuhusu mahitaji yako mahususi.
  • FEMA hufanya kazi na kila mtu - wapangaji na wamiliki wa nyumba - kwa msingi wa kesi baada ya kesi.

Usaidizi Mwingine Unapatikana kwa Kupigia 2-1-1

United Way 211 huunganisha watu binafsi wenye mahitaji ambayo hayajatimizwa kwa programu za usaidizi kupitia mashirika ya kujitolea na ya kidini. Yeyote aliyeathiriwa anayehitaji usaidizi wa ziada anapaswa kupiga simu 2-1-1 kwa usaidizi au atembelee http://211helps.org.

Tovuti ya recovery.mo.gov  pia rasilimali za ziada na taarifa kuhusu usaidizi wa majanga huko Missouri.

Makataa ya Kutuma Maombi ya FEMA ni tarehe 7 Oktoba 2022

Wapangaji na wamiliki wa nyumba katika Jiji la St. Louis, Kaunti ya St. Louis na Kaunti ya St. Charles ambao waliathiriwa na mafuriko Julai 25-28 wanaweza kutuma maombi ya usaidizi wa majanga ya FEMA.

Tuma maombi mtandaoni katika DisasterAssistance.gov, kwa kupiga simu 800-621-3362 au kwa kutumia programu ya simu ya FEMA.

Ikiwa unatumia huduma ya relay, kama vile video relay (VRS), simu iliyo na maelezo mafupi au huduma nyingine, pea FEMA nambari ya huduma hiyo. Waehudumu wa nambari ya usaidizi wanapatikana kutoka saa kumi na mbili asubuhi hadi saa nne usiku (6 a.m. to 10 p.m.) kila siku. Bonyeza 2 kwa Kihispania. Bonyeza 3 ili kupata mkalimani anayezungumza lugha yako.

Usimamizi wa Biashara Ndogo Marekani (SBA)

Mikopo ya majanga yenye riba nafuu kutoka kwa Usimamizi wa Biashara Ndogo Marekani (SBA) inapatikana kwa wafanyabiashara na wakazi wa Missouri kufuatia dhoruba za Julai. Ili kuzingatiwa kwa usaidizi wote wa majanga, waombaji lazima wajisajili kwanza na FEMA. Kisha wanaweza kutuma maombi mtandaoni kwenye tovuti salama ya SBA: https://disasterloanassistance.sba.gov/.

Wawakilishi wa SBA watasaidia wamiliki wa biashara na wakazi kutuma maombi katika vituo vya usaidizi wa majanga. Kwa orodha ya maeneo, au kupokea maelezo ya ziada ya usaidizi wa majanga, tembelea tovuti ya SBA katika www.sba.gov/disaster.

Waombaji wanaweza pia kupigia simu Kituo cha Huduma za Wateja cha SBA kwa 800-659-2955 au kutuma barua pepe kwa disastercustomerservice@sba.gov kwa maelezo zaidi. Kwa watu ambao ni viziwi, wasiosikia vizuri, au wenye ulemavu wa kuzungumza, tafadhali piga 7-1-1 ili kupata huduma za telecommunications relay.

Kituo kifuatacho cha Usaidizi wa Biashara cha SBA (BRC) kilifunguliwa Jumatatu, Agosti 15:

Urban League of Metropolitan St. Louis, Inc.

1408 N. Kingshighway Blvd.

Orofa ya pili, Room # 219

St. Louis, MO  63113

Saa na Siku za Uendeshaji: saa tatu asubuhi (9 a.m) – saa kumi na mbili jioni (6 p.m.), Jumatatu-Ijumaa

Kwa masasisho, tufuate kwenye Twitter @MOSEMA na @FEMARegion7.

Pata habari mpya kwa Recovery.MO.gov na FEMA.gov/disaster/4665.

Usaidizi wa majanga unapatikana bila kuzingatia rangi, dini, utaifa, jinsia, umri, ulemavu, ujuzi wa Kiingereza au hali ya kiuchumi.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho