Pata Ushauri kuhusu Kurekebisha Nyumba Lowe iliyoko Queens Novemba 1-6

Release Date Release Number
016
Release Date:
Oktoba 29, 2021

NEW YORK – Watu wa New York wanaporekebisha na kujenga upya nyumba zao, FEMA imeshirikiana na duka la Lowe la kuboresha nyumba huko Queens ili kutoa maelezo na vidokezo bila malipo kuhusu jinsi ya kufanya nyumba zilizoharibiwa na majanga ya asili kuwa imara na salama zaidi.

Wataalamu wa FEMA watapatikana katika eneo lililoorodheshwa hapa chini ili kujibu maswali na kutoa vidokezo na mbinu za kujenga nyumba zinazostahimili hatari ili kusaidia kuzuia au kupunguza uharibifu kutokana na majanga. Habari nyingi zinalenga jinsi ya kujifanyia kazi yako mwenyewe na wakandarasi wa jumla.

Washauri wa FEMA wa Kupunguza Hatari wanapatikana Jumatatu, Novemba 1 hadi Jumamosi, Novemba 6:

Lowe’s

253-01 Rockaway Blvd.

Rosedale, NY 11422

Masaa: saa 3 asubuhi hadi 12 jioni.

Vijitabu vya marejeleo bila malipo vyenye maelezo kuhusu kulinda nyumba kutokana na uharibifu wa mafuriko pia vitapatikana kwa walionusurika. Habari zaidi kuhusu kulinda mali inaweza kupatikana katika fema.gov/emergency-managers/risk-management.

Kwa taarifa za hivi karibuni kuhusu juhudi za kushughulikia Janga jijini New York, tembelea fema.gov/disaster/4615. tufuate kwenye Twitter twitter.com/femaregion2 na facebook.com/fema.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho