Pata Ushauri wa Kukarabati Makao Yako kati ya Oktoba 25 na 30 katika Maduka ya Lowe Kisiwani Staten

Release Date Release Number
013
Release Date:
Oktoba 22, 2021

NEW YORK – Huku wakazi wa New York wakiendelea kukarabati makao yao, FEMA wamejiunga na maduka ya Lowe Kisiwani Staten kutoa taarifa za bure na ushauri wa jinsi ya kuhakikisha kwamba nyumba zilizoharibiwa na mikasa asilia zinabaki kuwa thabiti na salama.  

Wataalamu wa FEMA watakuwepo katika eneo lililotajwa hapa chini ili kujibu maswali na kutoa ushauri na mbinu za kujenga makazi ambayo yanaweza kustahimili mikasa na kupunguza uharibifu wakati wa mikasa.  Taarifa nyingi zinalenga mambo ya kujifanyia mwenyewe na ufundi wa jumla.

Washauri wa FEMA kuhusu Namna ya Kupunguza Makali ya mikasa wanapatikana kuanzia Jumatatu, Oktoba 25 hadi Jumamosi, Oktoba 30:

Katika Maduka ya Lowe

2171 Forest Ave.

Staten Island, NY 10303

Muda: Saa Tatu Asubuhi (9 a.m.) hadi Saa Kumi na Mbili Jioni (6 p.m.)

Vijitabu vya marejeleo bila malipo vyenye taarifa kuhusu namna ya kulinda makazi dhidi ya uharibifu unaotokana na mafuriko vitatolewa kwa waathiriwa. Taarifa zaidi kuhusu jinsi ya kulinda mali yako zinaweza kupatikana kupitia  https://www.fema.gov/emergency-managers/risk-management.

Kwa taarifa za hivi karibuni kuhusu juhudi za kutoa misaada kwa waathiriwa wa Kimbunga Ida, tembelea fema.gov/disaster/4615. Fuatilia taarifa zetu kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii kupitia twitter.com/femaregion2 na facebook.com/fema.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho