Ikiwa Bima Haitafidia Hasara Yako, Mashirika Mengine Yanaweza Kukusaidia

Release Date Release Number
010
Release Date:
Oktoba 7, 2021

NEW YORK – Wakazi wengi wa Jiji la New York waliopata hasara kutokana na Kimbunga Ida wanalindwa na mashirika yao ya bima.  Lakini hata bima nzuri zaidi yaweza isifidie kila hitaji, jambo linalosababisha kuwepo kwa miradi ya jimbo, serikali ya kitaifa na mashirika mengine yasiyo ya serikali.

FEMA wanaweza kukutumia barua ikikuarifu kuwa hustahiki kupata msaada wa kitaifa wa kusimamia mikasa au wakiomba utume habari zaidi.   

FEMA wanatoa misaada kwa waombaji kusimamia hasara ya vitu vyao visivyokuwa na bima au vilivyokatiwa bima ndogo kuliko thamani yake na mahitaji muhimu. Waombaji wanafaa kuwaarifu FEMA kuhusu Bima zote ambazo wamechukua ikiwa ni pamoja na bima ya vyakula, bima ya nyumba, bima ya gari, bima ya makazi ya kuhamisha, bima ya afya, bima ya kugharamia mazishi, n.k.

Waombaji wenye bima ni sharti waonyeshe stakabadhi zinazothibitisha malipo au fidia ya bima kabla ya FEMA kutathmini ikiwa wanastahiki kupata aina nyingine ya usaidizi ambao unaweza kusimamiwa na bima za mashirika ya kibnafsi.   

Sababu zinazofanya upokee barua ya maamuzi ya FEMA ni pamoja na:

  • Upangaji wako wa nyumba haujathibitishwa;
  • Umiliki wa mali iliyoharibiwa haujathibitishwa;
  • Vitambulisho vya mwombaji havijathibitishwa;
  • FEMA hawakupokea stakabadhi za fidia ya bima. .

Unapaswa kusoma barua hiyo kwa makini ndio uweze kutoa habari au stakabadhi zinazohitajika na FEMA.

Ukiwa na swali lolote kuhusu barua hiyo au maamuzi ya FEMA, kuwa tayari na nambari yako ya usajili ya FEMA utakapopiga simu kwa Nambari ya HUDUMA ya FEMA kupitia 800-621-3362 (711/VRS).  Laini za simu hufanya kazi kuanzia saa mbili asubuhi (8 a.m.) hadi saa moja jioni (7 p.m.) siku saba za wiki, na wahudumu wanaweza kukuunganisha na mtaalamu anayezungumza lugha yako. Ikiwa unatumia nambari au laini ya simu ya wasiosikia/walemavu (relay call) kama vile huduma ya relay ya video, huduma ya simu ya maandishi (captioned telephone) au huduma nyingine, wape FEMA nambari ya huduma hiyo.

Kwa mujibu wa sheria za Marekani, FEMA hawawezi kuwalipa watu binafsi au familia zaidi ya mara moja kwa hasara zinazofidiwa na bima.  

Ikiwa una bima, unapaswa kuwasiliana na shirika lako la bima kuandikisha madai mara moja uombe stakabadhi zinazoonyesha fidia yako ya bima, mafao, na malipo, stakabadhi zinazoonyesha bayana ni kitu gani kimechukuliwa bima na kinapewa fidia katika madai yako. Kisha tuma habari hizo kwa njia ya posta kutumia anwani: FEMA, Individuals & Households Program, National Processing Service Center, P.O. Box 10055, Hyattsville, MD 20782-7055, au kutumia fax kwa nambari 800-827-8112. Kumbuka kuandika nambari yako ya usajili ya FEMA kwenye stakabadhi zote.

Unaweza kukata rufaa kuhusu maamuzi yoyote ndani ya siku 60 kutoka siku ya kuandikwa kwa barua ya maamuzi ya FEMA. Maelekezo ya kukata rufaa yanapatikana katika barua ya FEMA.

Unahimizwa kurejesha maombi yako ya mkopo wa Usimamizi wa Biashara Ndogo Ndogo wa Marekani (U.S. Small Business Administration—SBA) ikiwa ulipokea. Hii ni hatua muhimu ili uweze kufikiriwa katika aina nyingine za misaada ya mikasa. Unaweza kutuma maombi yako ya SBA kupitia kiungo hiki https://DisasterLoanAssistance.sba.gov au kwa taarifa zaidi, piga simu kwa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha SBA kutumia 800-659-2955. Aidha unaweza kutembelea Kituo chochote cha Kushughulia Mikasa. Unaweza kupata vituo hivi kupitia DRC Locator (fema.gov).

Siku ya mwisho ta kutuma maombi ya misaada ya mikasa ya FEMA ni Jumapili, Disemba, 5.

Kwa taarifa zaidi kuhusu masharti ya bima wakati wa mafuriko kwa wanaopokea misaada ya mikasa ya kitaifa, tembelea https://www.fema.gov/sites/default/files/2020-05/FloodInsuranceRequirements-080119.pdf. Kupata habari zaidi mtandaoni pamoja na vijitabu vya FEMA vinavyoweza kupakuliwa, tembelea DisasterAssistance.gov kisha ubofye “Information.”

Kwa rufaa kwenda kwa mashirika yanayosaidia katika mahitaji mahususi ya jamii, piga simu 211 au temebelea https://www.211nys.org/contact-us. Kwa wakazi wa Jiji la New York City, piga simu 311.

Wizara ya Afya na Huduma za Kijamii na Matumizi ya Dawa za Kulevya na Usimamizi wa Huduma za Afya ya Akili ya Marekani imeanzisha Nambari ya Usaidizi wa Mikasa. Huduma hii ya bure ya kusaidia wakati wa mikasa inapatikana saa na siku zote za wiki (24/7) kupitia 800-985-5990 kwa waathiriwa wa mikasa wanaopitia matatizo ya kiakili. Watumiaji wa Lugha ya Ishara Marekani wanaweza kuwasiliana kutumia huduma hiyo kwa simu ya video kupitia nambari hii 800-985-5990, au kwa kuchagua “ASL Now” upande wa kulia wa wavuti hii Disaster Distress Helpline-ASL Now.

Kwa taarifa za hivi karibuni kuhusu juhudi za kutoa misaada kwa waathiriwa wa Kimbunga Ida, tembelea fema.gov/disaster/4615. Fuatilia taarifa zetu kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii kupitia twitter.com/femaregion2 na facebook.com/fema.

Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho