Jukumu la Usimamizi wa Biashara Ndogo ya Marekani katika Urejesho

Release Date:
Agosti 4, 2023

FEMA mara nyingi huwatuma manusura wa majanga kwa Usimamizi wa Biashara Ndogo ya Marekani (SBA) ili kutuma maombi ya mikopo ya majanga yenye riba nafuu. Mikopo ya majanga ni sehemu muhimu ya msaada wa serikali, na inaweza kusaidia wamiliki wa nyumba, wapangaji, biashara za ukubwa wowote na baadhi ya mashirika yasiyo ya kibiashara kurejelea hali ya awali. 

Unapotuma ombi la msaada wa majanga ya FEMA, unaweza kutumwa kwa SBA

  • Mikopo ya majanga ya SBA ndio chanzo kikubwa zaidi cha fedha za misaada ya serikali baada ya majanga kwa walionusurika. SBA inatoa mikopo ya majanga ya muda mrefu, yenye riba nafuu kwa biashara za ukubwa wowote, mashirika ya kibinafsi yasiyo ya kibiashara, wamiliki wa nyumba na wapangaji.
  • Mikopo ya majanga ya SBA ina masharti yanayofaa sana yenye viwango vya riba visivyobadilika, uahirishaji wa malipo ya moja kwa moja kwa miezi 12 na riba ya 0% kwa miezi 12 ya kwanza.

Mikopo ya SBA inaweza kuwa sehemu muhimu ya urejesho wako

  • Kutuma maombi ya mkopo wa SBA huruhusu FEMA kukuzingatia kwa aina nyingine za misaada, ikijumuisha uharibifu wa magari, vifaa muhimu vya nyumbani na gharama zingine zinazohusiana na majanga.
  • Haulipishwi kutuma maombi, na si lazima ukubali mkopo ikiwa umeidhinishwa.
  • Ukiamua kutokubali mkopo, unaweza kuomba kukubaliwa tena ndani ya miezi sita. Unaweza kutuma ombi lako tena ukigundua uharibifu zaidi au kama malipo yako ya bima hayatoshi kulipia ukarabati.
  • Ikiwa SBA itakupata hustahili, wanaweza kukurejesha kwa FEMA, kisha inaweza kukutathmini kwa ajili ya msaada wa ziada.

Jenga tena kwa nguvu zaidi

  • Misaada ya FEMA na mikopo ya majanga ya SBA hufanya kazi pamoja kurekebisha uharibifu na kuendeleza urejeshaji wako.
  • Mikopo ya majanga ya SBA inaweza kutumika kufanya uboreshaji wa mali unaoondoa uharibifu wa siku zijazo au unaoweza kuokoa maisha. Mikopo ya majanga inaweza kuongezwa hadi 20% kwa ajili ya kuboresha majengo ili kupunguza uharibifu wa siku zijazo.
  • Kwa habari zaidi kuhusu SBA, piga simu kwa Kituo cha Huduma za Wateja cha SBA kwa 1-800-659-2955 (piga 7-1-1 ili kupata huduma za mawasiliano ya simu ya walemavu) au barua pepe DisasterCustomerService@sba.gov
  • Kuomba mkopo wa majanga ya SBA, tembelea DisasterLoanAssistance.sba.gov.
  • Kutuma maombi ya msaada, tembelea DisasterAssistance.gov, pakua FEMA App au piga simu kwa laini ya msaada ya FEMA kwa 1-800-621-3362. Ikiwa unatumia huduma ya usambazaji kama vile huduma ya usambazaji video (VRS), huduma ya simu iliyo na maelezo mafupi au nyinginezo, pea FEMA nambari yako ya huduma hiyo unapotuma ombi.
    • Ili kupata Kituo cha Msaada wa Majanga, ambapo wataalamu wa FEMA wanaweza kukusaidia kutuma ombi na kujibu maswali ana kwa ana, tembelea fema.gov/drc.
Tags:
Ilisasishwa mara ya mwisho