Ukaguzi wa Nyumbani

Tayarisha

Wakati wa

Baada ya

Msaada wa Ziada

Baada ya kuwasilisha ombi la msaada wa janga, lazima FEMA ithibitishe uharibifu wako uliosababishwa na janga kupitia ukaguzi wa ana kwa ana au wa mbali. Katika kipindi cha siku chache wafanyakazi na wakaguzi wa FEMA wanaweza kupiga simu kutoka kwa nambari ya simu isiyojulikana au iliyozuiliwa na kufanya majaribio kadhaa ya kujadili uharibifu wako uliosababishwa na janga.

Ukaguzi unaweza kufanywa tu wakati mwombaji (wewe) au mwombaji-mwenza yupo. Ikiwa mwombaji au mwombaji-mwenza hawezi kukutana na mkaguzi, mtu wa tatu anaweza kuteuliwa kwa maandishi na kuidhinishwa kabla ya muda uliopangwa na tarehe ya ukaguzi.

Ikiwa nyumba haiwezi kufikiwa, mkaguzi anaweza kukutana na mwombaji katika kizuizi au eneo lisilohusiana ili kuthibitisha ukaaji na/au umiliki.

Graphic
Within 10 Days After Applying Graphic

Kujitayarisha kwa Ajili ya Ukaguzi Wako

Usisubiri ukaguzi ufanyike ili ufanye yafuatayo:

  • Wasilisha dai kwa kampuni yako ya bima, ikiwa una bima.
  • Anza kufanya usafi sasa, ikiwa ni salama kufanya hivyo.
  • Piga picha za uharibifu wowote.
  • Andika orodha ya hasara zako.
  • Weka risiti zote ili kuthibitisha gharama zilizosababishwa na janga.

Kuratibu Ukaguzi Wako

alert - warning

Kumbuka kwamba wafanyakazi na wakaguzi wa FEMA wanaweza kupiga simu kutoka kwa nambari ya simu isiyojulikana au iliyozuiliwa na kufanya majaribio kadhaa katika kipindi cha siku chache.

Iwapo FEMA haitaweza kuwasiliana nawe ili kuthibitisha uharibifu wako, utatumiwa barua ya ilani na ombi lako halitaweza kushughulikiwa zaidi—ili kuendelea lazima upige simu kwa laini ya Msaada ya FEMA (800-621-3362) ili kuhakikisha habari zako za mawasiliano na kuthibitisha uhitaji wako wa msaada. Usitume tena au kuunda ombi jipya wakati wowote ambapo ombi lako la msaada wa janga linashughulikiwa. Unaweza kuangalia hali ya ombi lako au kusoma barua zozote za FEMA kwa kuenda kwa akaunti yako ya DisasterAssistance.gov.

Maelezo ya Kukusanya kwa Ajili ya Ukaguzi Wako

Unapaswa kuwa na maelezo yafuatayo tayari wakati wa ukaguzi:

  • Kitambulisho cha picha
  • Uthibitisho wa umiliki au ukaaji, iwapo utaombwa na mkaguzi
  • Orodha ya wakazi wa nyumba walioishi nyumbani wakati wa janga
  • Uharibifu wote wa mali uliosababishwa na janga
  • Mkataba wako wa bima na hati zozote za ziada zilizoombwa na mkaguzi

Wakati wa Ukaguzi Wako

Graphic
A blue fema inspector with a phone to his ear

Wakaguzi wa FEMA wamezoezwa kutambua uharibifu uliosababishwa na janga, lakini hawaamui ikiwa utapata msaada.

Wanachunguza na kurekodi uharibifu ambao unaweza kustahili ndani ya Mpango wa Watu Binafsi na Familia, ambao ni tofauti na tathmini zinazofanywa na warekebishaji wa bima au programu nyingine za msaada wa janga, kama vile Usimamizi wa Biashara Ndogo wa Marekani.

Kulingana na kiasi cha uharibifu, ukaguzi unaweza kuchukua hadi dakika 45 kukamilika.

Maandalizi Wakati wa Ukaguzi Wako

Maandalizi yanayofaa, yakitia ndani utafsiri na wakalimani wa ASL, yatapatikana ili kuhakikisha mawasiliano yanayofaa na waathiriwa walio na ustadi mdogo wa Kiingereza, waathiriwa wenye ulemavu, na watu wengine wenye mahitaji ya kufikia na kufanya kazi.

Unaweza kumwalika mtu, kama vile mshiriki wa familia, jamaa au rafiki, ili kusaidia katika kuwasiliana na mkaguzi.

Baada ya Ukaguzi Wako

Utapokea maelezo yanayofafanua uamuzi wa kustahili msaada wa FEMA ndani ya siku 10 baada ya ziara ya mkaguzi.

Kuamua Kustahili

Iwapo umebainika kwamba unastahili Msaada, unaweza kupokea hundi ya Hazina ya Marekani au amana ya moja kwa moja kulingana na ulichochagua wakati wa kuwasilisha ombi lako.

Iwapo umebainika kwamba hustahili Msaada au ombi lako halijakamilika, unaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo ndani ya siku 60 na/au uombe fursa ya kukamilisha ombi hilo.

Msaada wa Ziada

Wakaguzi wa FEMA hawawezi kujibu maswali au kupata maelezo yako mara tu wanapokamilisha ukaguzi wako. Iwapo una maswali baada ya ukaguzi wako, tafadhali piga simu kwa Laini ya Msaada ya FEMA kwa 800-621-3362.

Habari za Ukaguzi wa Nyumbani

Ilisasishwa mara ya mwisho